Thursday, March 30, 2017

BREAKING;Mbunge lijualikali aachiwa huru

Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali yuko huru baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero. #Mwananchileo

Tuesday, March 28, 2017

Agizo la DC katika kata ya Moivaro

Kutokana nakuwepo kwa tatizo la kivuko katika kata ya Moivaro mkuu wa wilaya ya  Arusha ameagiza watendaji wahakikishe wanatengeneza kivuko cha muda ili kiweze kuruhusu mawasiliano wakati serikali ikijipanga katika ujenzi wa daraja la kisasa
Hata hivyo wananchi wamezungumzia suala la uwepo wa umeme mdogo pamoja na suala la machimbo ya moramu

Monday, March 27, 2017

Waziri aagiza Nay wa mitego aachiwe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego.

- Waziri ameishauri BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.


BREAKING;Wimbo wa Nay wa mitego wafungiwa

: Baraza la Sanaa Tanzania limeufungia Wimbo wa Wapo wa Nay wa Mitego na kutoa onyo kwa wanaosambaza au kutumia nyimbo zilizofungiwa kuwa ni kosa kisheria

Tuesday, March 21, 2017

Diwani wa Chadema Arusha amesema wanaompinga RC,DC na mkurugenzi nivichaa


BREAKING;Diwani wa kata ya kimandolu CHADEMA  Rhyson Ngowi amesema wanaomkataza kufanya kazi na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqarro  na mkurugenzi wa jiji Athumani Kihamia pamoja  viongozi wengine ni vichaa na yeye anatekeleza ilani ya chama kilichopo madarakani

Amesema hua hapendi siasa za mafarakano na atawapa viongozi ushirikiano
#Ziara ya Dc Kimandolu



Friday, March 17, 2017

Tundu lisu alipowasili kwenye kituo cha AICC

UPDATE;Mgombea urais wa TLS Tundu Lisu  amewasili katika kituo cha mikutano cha kimataifa Arusha AICC ni Mara baada ya kupata dhamana siku ya Leo baada yakutoka mahakamani