Pages

Friday, January 17, 2014

KIKWETE ASOGEZA MBELE MUDA WA KUTANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI

8bf0b-k50
Taarifa tulizozipata hivi pude, zinadai kuwa, Rais Jakaya Kikwete amesogeza mbele muda wa kutangaza baraza lake la mawaziri kujaza nafasi ya waziri aliyejiuzulu na wale wanaoitwa “mzigo.”
Taarifa zinasema, Rais Kikwete atatangaza baraza lake la mawaziri mwishoni mwa wiki.
Vyanzo vya taarifa kutoka Ikulu vinamnukuu Rais akisema, “Nimeshauriwa na watu wema kabisa, kwamba nisubiri kidogo kutangaza baraza angalau kumalizia msiba wa aliyekuwa waziri wa fedha,” Dk. William Mgimwa.
Wakati tunaendelea kusubiri, baadhi ya wanasiasa, mawaziri, wabunge na wananchi wengine wa kawaida, hasa wanachama wa CCM wanaendelea kupara presha kwa kujiuliza; nani atakuwamo na nani hatakuwamo.

No comments:

Post a Comment