MADIWANI ARUSHA WASIKITISHWA NA UTENDAJI MBOVU WA WA JIJI
BARAZA la madiwani wa jiji la Arusha, limedai kusikitishwa na
uchelewaji wa kutotekelezwa kwa maazimio yanayopitishwa na baraza hilo
mra kwa mara na hivyo kuafikiana kutohudhuria vikao vyovyote vya
baraza mpaka utekelezaji wa maagizo mbalimbali waliyotoa
yatakapotekelezwa.
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, Meya wa jiji la
Arusha Gaudence Lyimo alisema watendaji wa Halmashauri ya Jiji la
Arusha wamekuwa wakipuuzia maagizo yanayotolewa na baraza la madiwani
na badala yake kutoa majibu yasiyokuwa sahihi.
Alisema katika vikao vya baraza hilo vilivyofanyika kuanzia mwaka 2008
kuhusu kugawanywa kwa baadhi ya kata kutokana na ukubwa wake na
baadhi ya wananchi kukosa huduma za msingi ikiwa ni pamoja na
maji,elimu na miundo mbinu Kata za Moshono, Sokoni One ,Olasiti,
Elerai,Terrat, na Sombetini.
“kwa kweli hapa hatuwezi kuelewana bila kutekelezwa kwa maazimio
ambayo tumeyajadili kwa pamoja hatutaweza kushiriki vikao vijavyo kama
hakuna utekelezaji” alisema Lyimo
Naye Mbunge wa viti Maalum Mary Chatanda akizungumzia adha ya
michango michango ambayo imekuwa ikitozwa na wakuu wa shule mbalimbali
za msingi na Sekondari jijini Arusha kwa wanafunzi wanaoanza kidato
cha kwanza na darasa la kwanza alisema.
“ michango katika shule hizi imekuwa ikiweka matabaka kati ya watoto
wenye uwezo na masikini jambo ambalo sio lengo la Serikali la
kuanzisha shule za Kata na hili mheshimiwa mwenyekiti limenikuta
lakini tukumbuke kuwa sio wote wenye uwezo wa kulipa fedha hizi
kwamaana mimi nitaweza lakini je jirani yangu ambaye hana uwezo
atafanyaje?” alisema Chatanda
Akijibu tatizo hilo la michango, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,
Gerald Mollel alisema Halmashauri yake imeteua wajumbe wanaopitia
katika shule mbalimbali ili kubaini lengo la michango hiyo shuleni.
Aidha Baraza la madiwani limemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji
kufuata taratibu za kufunga Sekondari ya Kinana kufuatia kukosa huduma
ya hosteli kwa ajili ya wanafunzi kukaa kutokana na umbali mrefu wa
wanafunzi kwenda shuleni hapo.
“Mbali ya Kinana tunaagiza pia shule ya Corona iendelee kufungwa hadi
hapo ujenzi wake utakapokamilika kwa kuwa na yenyewe iko mbali sana,
binafsi nimekuwa nikibeba wanafunzi wa Kinana wanatembelea umbali wa
zaidi ya KM14 lazima ijengwe hosteli pale,”alisema Meya Lyimo.
Maagizo mengine yanayoelezwa kushindwa kutekelezwa na watendaji wa
Halmashauri hiyo ni pamoja na ujenzi wa zahanati ya Moshono, vyanzo
vya mapato ya Halmashauri ya jiji la Arusha, kutoitishwa kwa vikao vya
kamati za madiwani na kuitwa kwenye vikao kwa watendaji mbalimbali wa
Halmashauri waliohamishwa kujibu hoja muhimu zinazowahusu.

No comments:
Post a Comment