Chadema kimeshindwa kwa mengi uchaguzi madiwani
Takwimu mbalimbali nchini zinaonyesha kuwa wapo
vijana zaidi ya milioni tatu ambao hawajaandikishwa katika daftari hilo.
Mbali na hao wapo waliopoteza vitambulisho vya kupiga kura, waliohama
maeneo yao ya awali na wengine wenye kasoro mbalimbali na hivyo kupoteza
sifa za kupiga kura. Sababu ya pili ni wananchi kuwa na mwamko mdogo wa
kujitokeza siku ya kupiga kura. Jambo hili linasababishwa na mambo
mengi ikiwa ni pamoja na kutotolewa kwa elimu ya kutosha ya uraia.
Lipo suala la mgogoro ndani ya Chadema. Jambo hili
linatajwa kuwa sababu ya chama hicho kutofanya vizuri lakini binafsi
sidhani kama ni sababu kuu, ingawa inaweza kuchangia kwa kiasi fulani.
Jambo jingine ni CCM kuwa na viongozi wapya ambao
ni Makamu Mwenyekiti Philip Mangula na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana.
Hawa wanaweza kuwa chachu ya ushindi wa CCM kwa sababu tangu wakabidhiwe
majukumu yao mapya wamekuja na mikakati ambayo imekisaidia chama hicho,
ukiwemo ule wa kuibua hoja za kutoswa kwa mawaziri mzigo. Ikumbukwe
kuwa ziara ya viongozi hao katika mikoa mbalimbali nchini ilisababisha
mambo yaliyokuwa yamelala hasa maeneo ya mipakani, kero zilizokuwa
zikiwakabili wakulima na wafugaji kupatiwa ufumbuzi kwa muda mfupi.
Jambo jingine lililosababisha Chadema kishindwe
kufanya vyema ni kutojikita zaidi maeneo ya vijijini kama ilivyo kwa
CCM. Hilo utalibaini katika kata ambazo chama hicho kimeshinda, zote
zipo mjini wakati CCM imeshinda kata nyingi zilizopo maeneo ya vijijini.
Siyo katika uchaguzi huo tu hata ule wa 2010, CCM kimekosa baadhi ya
majimbo mjini kimeshinda vijijini huku Chadema kikiibuka na ushindi
mkubwa maeneo ya mjini.
Pamoja na hayo Chadema kinatoa upinzani na
kitaendelea kutoa upinzani kwani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010
hakikuweka mgombea Kata ya Njombe Mjini. Katika uchaguzi wa Februari 18
kimeweka mgombea na kimeibuka na ushindi. Mwaka 2010 katika Kata ya
Mpwayungu mkoani Dodoma Chadema kilipata kura 602 na CCM 1812. Katika
uchaguzi wa Februari 8, Chadema kimepata kura 555 na CCM kura 872.
Hata Kata ya Ubagwe mwaka 2010, CCM kilipita bila
kupingwa. Uchaguzi wa mwaka huu CCM kimepata kura 329 na Chadema 215.
Siasa ni ushindani na ndiyo maana wapo wanaotaka wapinzani waungane ili
kuing’oa CCM madarakani. Kama hilo halitawezekana basi vyama vya
upinzani vinatakiwa kujipanga kwasababu kuking’oa chama chenye dola siyo
mkazi rahisi.
No comments:
Post a Comment