Pages

Thursday, March 6, 2014


BUNGE MAALUM LA KATIBA LAAHIRISHWA KUTOKANA NA VURUGU.

Mwenyekiti wa Muda wa Bunge  la Katiba Mh. Pandu Kificho ameahirisha Semina ya kujadili Kanuni za Bunge Maalum la Katika Kutokana na Vuruguru na Hali ya Kutokuelewana Kati ya Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mh Ole Sendeka Kutoleana maneno na Mbunge Mwenzake wakati Mbunge Huyo alipohoji kuhusu Kanuni hizo.
 
Bunge Maalumu la Katiba linalokutana mjini Dodoma leo limeingia dosari kufuatia vurugu kubwa zilizotokea ndani ya ukumbi wakati wajumbe wakichangia maoni katika kifungu cha 58 cha kanuni za uendeshaji, hali iliyosababisha kuahirishwa kwa muda.
Chanzo cha vurugu hizo kilianzia kwa Waziri wa Sheria na Katiba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Abubakari Hamisi Bakari alipomweleza mwenyekiti kuwa jina la Christopher Ole Sendeka halikuwa katika orodha ya majina ya wachangiaji.


Bakari amesema kitendo kama hicho ambacho kilimfanya mjumbe mwingine Ummi Mwalimu kuzuiwa kuchangia kingeweza kulifanya Bunge likaendelea kujadili kanuni hadi miezi sita kwani tabia ya kuruhusu majina inafanywa na Sekretarieti kinyemela.
Hali hiyo imemkera Ole Sendeka na kulazimika kutoa maneno ya kejeli kwa Bakari akieleza kwamba anazijua sheria kuliko waziri huyo huku akimtuhumu kuwa ana ajenda yake ya siri katika kukwamisha mchakato huo.
Kauli ya Ole Sendeka illipua hisia za wengi na karibu nusu ya wajumbe walisimama na kuanza kupigizana kelele wakimtaka aombe radhi hatu ambayo iliungwa mkono na mwenyekiti wa muda wa bunge hilo Pandu Ameir Kificho.
Hata hivyo, hali ilikuwa mbaya zaidi pale alipopewa nafasi bakari ambaye alikejeli kuwa anazijua sheria vizuri kwani tangu mwaka 1980 amekuwa katika mabunge hayo kuliko Ole Sendeka ambaye ametokea Simanjiro miaka 10 iliyopita.
Kufuatia mvutano huo utulivu wa Bunge ulipotea, kwani kila upande ulianza kupiga kelele na kuwasha vipaza sauti  hali iliyosababisha Kificho kuahirisha shughuli za bunge hilo hadi saa 10 hii jioni.
 

No comments:

Post a Comment