Pages

Sunday, July 10, 2016

meya kalisti amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa mameya na wenyeviti pamoja na mjumbe wa kamati kuu ya chadema

Meya Kalisti Lazaro wa Jiji la Arusha amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mameya na Wenyeviti wote wa Halimashauri wanaotokana na CHADEMA.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob, ameteuliwa kuwa Katibu wa Umoja huo wa Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini Mosses Matiko Misiwa ameteuliwa kuwa mnadhimu wa Umoja huo wa Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri zote zinazoongozwa na CHADEMA.
Note that:
Kwa kuchaguliwa kwao, kunawafanya kuwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa.
Diwani,
Mhe.Francis M. Garatwa.


hapa chini ni maneno aliyoandika kwenye ukurasa wake wa facebook

Nawashukuru sana wenyeviti wa Halimashauri mbalimbali kupitia CHADEMA na Mameya wote wa chadema Tanzania nzima kwa kuniamini na kunipigia kura niwe Mwenyekiti wa baraza la Madiwani Tanzania nzima Nakua mjumbe rasmi wa kamati kuu ya CHADEMA, Mungu awabariki sana.

No comments:

Post a Comment