Sunday, May 28, 2017

Mkurugenzi kihamia avunja rekodi K.K.K.T afanikisha upatikanaji wa mil 39 viongozi wambariki




Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athuman Kihamia ameweza kushiriki katika harambee yakuchangia maenedeleo ya mtaa pamoja kanisa la KKKT usharika wa Enaboishu mtaa wa loruvan nakufanikiwa kupatikana fedha zaidi ya milion 39 ambazo zitatumika katika shuhuli mbalimbali

Awali baada yakufanikisha suala hilo viongozi wa dini walipata nafasi yakumuombea sala malumu kwa jinsi alivyojitoa katika masuala ya maendeleo

Pamoja na hayo kihamia amewaomba waliotoa ahadi kutimiza ili kuweza kuharakisha maendeleo
Hata hivyo ameongozana na viongozi mbalimbali akiwemo mfanyabiashara Philemon Moleli

Thursday, May 18, 2017

Mkurugenzi wa jiji Arusha asema meya na naibu meya wamesababisha hasara baada yakutokuhudhuria vikao

Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athuman kihamia amesema leo kikao cha robo mwaka kupitia mirad ya maendeleo pamoja na shughuli nyingine za serikaki kimeshindwa kuendelea baada ya meya na naibu meya kushindwa kuhudhuria kikao bila kutoa taarifa

Kihamia amesema pamoja na hasara zilizotokea ni pamoja na chakula kilichokuwa kimeagizwa pamoja na mambo mengine

Hata hivyo amesema ataendelea kutekeleza majukumu yake kwa ajili yakuwaletea maendeleo wananchi

Saturday, April 8, 2017

Mimi ni mzima wa afya- Roma Mkatoliki

BREAKING NEWS;'Mimi ni mzima kabisa kiafya' @roma2030 akizungumza na waandishi muda mfupi baada ya kufanyiwa vipimo hospitali ya Mwananyamala, amesema atazungumza  mengi Jumatatu

Wednesday, April 5, 2017

Jiji la Arusha limetoa bure bima ya afya kwa walemavu 351



Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athuman Kihamia amesema Jumla ya walemavu 351 waliopo katika jiji la Arusha watatibiwa nakupewa huduma za afya bure kwa mwaka mzima kutokana na changamoto ambazo wamekuwa wakizipata

Thursday, March 30, 2017

DC Arusha azungumzia walivyofeka posho za madiwani Arusha


;Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqarro amesema miradi ya maji,elimu bure pamoja na huduma nyingine za kijamii zinazotolewa ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi nakuwataka wananchi kufanya kazi pamoja nakutoa ushirikiano kwa serikali

Hata hivyo amewataka wananchi wanaomiliki nyumba zao kwenda TRA kwa ajili ya uhakiki ili waweze kulipa kodi ili serikali iweze kupata mapato

Hata hivyo amegusia suala la posho za madiwani nakusema wataendelea kuzibana kwa kuwa walikuwa wanataka kujilipa shilingi elfu 80 za nauli za usafiri kinyume na utaratibu na watalipwa shilingi elfu 10 kwa kata za karibu na shilingi elfu 20 kwa kata za mbali na jiji