Hatimaye bunge
la afrika mashariki limeweza kupiga kura ambazo zimeweza kufikia zaidi ya
theluthi mbili nakuweza kumuondoa Dr. Margaret Nantongo Zziwa
katika nafasi ya spika wa bunge hilo
Mapema jana asubuhi
Bunge liliweza kusikiliza ripoti ya Kamati ya Kisheria Kanuni na Haki
juu ya uchunguzi wa malalamiko ya kuondolewa Spika kutoka
katika kiti hicho ambapo ameodolewa
madarakani na wabunge wa Afrika Mashariki,na Kumpa saa 24 kukabidhi ofisi hiyo
Aliyekuwa spika wa bunge la Afrika Mashariki Dr magreth zziwa
Bunge hilo limeketi huku likiwa chini ya uenyekiti na Afisa Mkuu, Mhe Chris Opoka Okumu ambaye alichaguliwa na cheo cha juu mwendo kwa ajili ya kuondolewa Spika juu ya Novemba 26, 2014 katika kikao cha mjini Nairobi. Rt. Mhe Zziwa hakuwepo wakati wa mjadala huo
Kwa upande wa
mtoa hoja ya kun’golewa kwa spika wa bunge hilo peter mathuki kutoka kenya
kenya hapa anaelezea hali ilivyokuwa baada ya jambo hilo kufanikiwa
Jumla ya wabunge 39 walishiriki katika kikaao cha bunge hilo
kilichofanyika asubuhi ya leo chini ya aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa bunge hilo
idadi ya kura zilizounga mkono kuondolewa kwa spika huyo ni 36, mbili
zilisema hapana na moja kuharibika.
Hata hivyo bunge hilo litapiga kura siku ya ijumaa kumchagua spika mwingine wa bunge hilo ambaye
atatokea uganda
No comments:
Post a Comment