Mchezaji wa timu ya taifa ya Cameroon Assou Ekotto akimtoka mshabuliaji wa timu ya Taifa Stars katika mchezo wa Kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo Taifa Stars ikiibugiza timu ya Cameroon Goli 1-0 na kutoka uwanjani kifua mbele.
Goli la timu ya Taifa Stars limefungwa na mchezaji Mwana Samata baada ya kupokea krosi kutoka kwa mchezaji mwenzake Domayo katika dakika ya 89 ya mchezo huo, Mbwana Samata anacheza mpira wa kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Lubumbashi nchini DRC CONGO.
Mchezaji wa timu ya Taifa Stars Salum Abubakar akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Cameroon Makoun Thierry katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo.
Mashabiki mbalimbali wa timu ya Taifa Stars wakishuhudia mchezo huo ambapo Taifa Stars imeifunga Cameroon Goli 1-0.
No comments:
Post a Comment