Mahakama kuu
kanda ya Arusha imemwachia kwa dhamana mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless
Lema mara baada ya kusomewa mashtaka yaliyokuwa yanamkabili kuhusiana na vurugu katika chuo cha uasibu .
Mheshiwa
Lema alikamatwa na jeshi la polisi mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kile
kinacholezwa kwamba ni tuhuma za uchochezi katika ghasia zilizotokea katika
chuo cha uasibu Arusha.
Akimsomea shitaka
hilo wakili wa serikali ELIANENYI NJIRO amesema kwa mujibu wa sheria mbunge Lema
amekiuka kifungu namba 390 cha sheria ya makosa ya uchochezi na kusababisha
vurugu.
Hata hivyo
mara baada ya shtaka hilo kusomwa mbele ya hakimu DEVOTA MSOFE mh: Lema
ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja na mdhamini mmoja ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi may 29
mwaka huu.
Akizungumza
na wandishi wa habari katika ofisi za chama cha Demokrasia na Maendelao
(CHADEMA) Mkoa wa Arusha ,mara baada ya kutoka mahakami hapo Mh: Lema amesema
hatua ya kunyimwa dhama imemwzesha kufahami keroi mbalimbali zinazowakabili
mahabusu ikiwa ni pamoja na msongamano mkubwa
katika mahabusu hizo.
Vurugu hizo
katika chuo cha uhasibu jijini arusha zilizosababishwa na tukio la kuuawa kwa
mwanafunzi mmoja, zimepelekea chuo hicho kufungwa kwa muda usiojulikana na
wanafunzi kurejea makwao.
No comments:
Post a Comment