Friday, May 10, 2013

UCHUNGUZI WABAINI: Wanawake Wanapenda Kufanya Ngono Zaidi Ya Wanaume




Tofauti na watu wengi wanavoamini kwa miono yao ya kwamba wanaume ndio wananaopenda ngono zaidi ya wanawake, uchunguzi wa hivi karibuni umepingana na mawazo ya walio wengi.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na posti ya Huffington, umebaini kwamba wanawake wengi walio kati ya miaka 25-65 wamekiri kwamba wanawake wana msukumo mkubwa unaowaendesha kutaka ngono, ila tatizo kubwa ni sababu ya kuwa na wanaume ambao hawashiriki ipasavyo kusaidia msukumo huo.

Hii inakuja kueleza kwamba, baadhi ya wanawake nao huwa wanahitaji na kuwa na msukumo wa kufanya mapenzi kama ambavyo wanaume hutaka au wakati mwengine msukumo wao huwa ni zaidi ya wanaume.
Baadhi ya wanawake hao wamesema kwamba bado wanahangaika bila kupata penzi la kutosha toka kwa wanaume zao.

Japokuwa posti hii haikusema ni nani hasa wa kulaumiwa, ila inachotaka kueleza moja kwa moja ni kwamba wanawake nao wana muamko wa kufanya mapenzi kama ule ambao wanaume wanaupata.

No comments:

Post a Comment