Wednesday, June 19, 2013

WABUNGE WANNE WA CHADEMA WAPEWA DHAMANA POLISI,HAWAJAFIKISHWA MAHAKAMANI

WABUNGE WANNE WA CHADEMA WAPEWA DHAMANA POLISI,HAWAJAFIKISHWA MAHAKAMANI

Wabunge waViti maalum Chadema,wakiwasili Mahakama ya Hakimu mkazi  Arusha leo kusikiliza kesi  

Mwanasheria wa Chadema,Mabere Marando(shoto)akiwa na Wakili wa kijitegemea wa jijini Arusha,Alute Mghwai

Mbunge wa Ubungo,John Mnyika(shoto)na Makamu mwenyekiti wa Chadema Zanzibar wakisubiri kusikilizwa kwa kesi

Mbunge wa Rombo mkoani Kilimanjaro,Joseph Selasini akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema(Bavicha) John Heche


Wabunge wanne wa Chadema,Tundu Lissu,Mustafa Akoonay,Joyce Mukyaa na Said Arfi wamepewa dhamana katika kituo cha Polisi cha jijini Arusha

Huku wabunge wa chama hicho walioko jijini hapa na wafuasi wa Chadema wakiwa wamejikusanya katika Mahakama ya Hakimu mkazi walipigwa na  butwaa kuona watu waliokuwa wakiwasubiri kufikishwa mahakamani baada ya kukamatwa na polisi jana jioni kutofikishwa kama ilivyokuwa imetangazwa na Kamishna wa Polisi,Paul Chagonja.

Watuhumiwa hao 67 walikamatwa jana kwa kile kilichodaiwa kukusanyika kwenye uwanja wa Soweto bila idhini ya mwenye uwanja ho AICC
                                                                                                                                             

No comments:

Post a Comment