WANAHABARI WATEMBELEA MRADI WA URANIUM WA MANRTA TANZANIA,NAMTUMBO MKOANI RUVUMA
Afisa wa Kitengo cha Usalama wa
Kampuni ya Mantra Tanzania inayoshughulika na Mradi wa Uchimbaji Madini
aina ya Uranium,uliopo kwenye Kijiji Mkuju,Wilayani Namtumbo Mkoani
Ruvuma,Fredrick Kriel akitoa mada ya maswala ya Usalama Mgodini wakati
wa Semina fupi kwa Baadhi ya Wanahabari waliofanikiwa kutembelea Mradi
huo uliopo pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seluu na kufahamu mambo
mbali mbali juu ya Madini hayo ya Uraniuam.
Afisa wa Kitengo cha Usalama wa
Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel akionyesha moja ya mambo
muhimu na yanayotakiwa kuzingatiwa kwa mtu yeyote awapo Mgodini.
Meneja Mkuu wa Maswala ya Usalama,
Afya, Mazingira na Ubora wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Cornelis Van Den
Berg akifafanua jambo kuhusu mradi huo wa Madini ya aina ya Uranium
wakati wa semina fupi na baadhi ya Wanahabari walioweza kutembelea Mgodi
huo leo,na kuweza kujionea na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Mgodi
huo.
Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa
Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Palangyo akielezea namna Kampuni yake
inavyoweza kutoa kipaumbele katika kusaidia jamii inayouzunguka mradi
huko.
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo
mbali mbali vya habari hapa nchini wakifatilia mada zilizokuwa
zikiwasilishwa na wahusika wa Mradi huo.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni
ya Montage,Teddy Mapunda ambaye ameambatana na wanahabari hao,na wa pili
kulia ni Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra
Tanzani,Khadija Palangyo.
Sehemu ya Mandhali ya Mahema ya maofisi ya Kampuni hiyo wakati huu wa Utafiti wa Madini ya aina ya Uranium.
Wanahabari hao wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wasimamizi wa Mradi huo.
Afisa wa Kitengo cha Usalama wa
Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel akitoa maelezo ya namna mambo
yanavyokuwa pindi wawapo kazini.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
Montage,Teddy Mapunda na kushoto ni Mwanalibeneke
No comments:
Post a Comment