AWUSA YAANZISHA ULIPIAJI WA ANKARA KUPITIA MITANDAO YA SIMU
Mamlaka
ya maji safi na maji taka jijini Arusha [AWUSA] wameanzisha huduma ya kulipa bili ya malipo ya Ankara kwa wateja kupitia mitandao yote ya simu za mikononi. Akizungumza na Nipashe mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Masoud Katiba katika maonyesho ya wakulima na wafugaji TASO nane nane,alisema kuwa mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Arusha limeamua kuweka huduma hiyo ili kuweza kulipa bili zake kwa wakati unaotakiwa. Aidha alisema kuwa sababu nyingine ya kuweka huduma hiyo ni ili kumrahisishia mteja wake katika kupunguza muda mwingi wakati wakulipa Ankara zake,na kutembea muda mrefu kuzifuata huduma hizo na kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza. Masoud aliongeza kuwa mitandao itakayotumika katika kurahisisha huduma za mamlaka ni pamoja na M-PESA,TIGO PESA,AIRTEL MONEY ambapo amesema mpaka sasa asilimia 10 ya wateja wameanza kulipia bili zao kwa kutumia mtandao wa M-PESA ambapo amesema ndani ya mitandao yote kuna namba maalumu ambazo mteja anaweza kuzitumia Aidha alibainisha kuwa njia hii itamsaidia mwanananchi kuokoa muda na fedha nyingi ambazo alikuwa akiutumia kwa ajili ya kwenda idara ya maji badala yake anatumia kwa kufanyia kazi nyingine. “tumeanzisha hii ili kumraisishia mteja kulipa bili yake kwa wakati nabila usumbufu wowote napia na sisi kama idara ya maji tunatakiwa tuende na wakati hasa katika kipindi hichi cha digital”alisema Masoud Alitoa wito kwa wananchi kuepuka na usumbufu wa kwenda kulipa bili zao za maji (Ankara)katika ofisi na badala yake watumie huduma hizi mpya. |
No comments:
Post a Comment