Thursday, August 8, 2013

BENKI YA FBME YATOA MKONO WA IDD KWA WATOTO YATIMA

DSCF0137
Meneja wa benki ya FBME LTD mkoa wa Arusha Ramadhani Lesso  akikabidhi misaada mbalimbali kwa mama mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Matonyok kilichopo Olasiti Bi.Emmy Sitayo kwaajili ya sikukuu ya  Idd El Fitiri,misaada hiyo inadhamani ya shilingi laki saba na nusu kwa vituo viwili pamoja na cha Abu-Abdulrahamani kilichopo Jr  jijini Arusha
 DSCF0160
Meneja wa benki ya FBME LTD mkoa wa Arusha Ramadhani Lesso  akikabidhi misaada mbalimbali kwa mama mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Abu-Abdulrahamani kilichopo Jr  jijini Arusha jana kwaajili ya sikukuu ya  Idd El Fitiri,misaada hiyo inadhamani ya shilingi laki saba na nusu kwa vituo viwili pamoja na cha Matonyok kilichopo Olasiti
DSCF0130
DSCF0128Afisa wa benki ya FBME Mnukwa Ally akiongea na watoto waishio katika mazingira magumu katika kituo cha Matonyok kilichopo Olasiti,mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali  iliyotolewa na benki hiyo kwaajili ya sikuu ya Idd El Fitiri
DSCF0142
Meneja wa benki ya FBME LTD Ramadhani Lesso akiongea na watoto waishio katika mazingira magumu katika kituo cha Matonyok kilichopo Olasiti,mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali  iliyotolewa na benki hiyo kwaajili ya sikuu ya Idd El Fitiri
DSCF0146
Hizi ni nguo zilizoanikwa chini katika kituo cha Abu-Abdulrahamani kilichopo Jr  jijini Arusha
DSCF0124
Mfanyakazi wa benki hiyo akisalimiana na watoto katika kituo cha Matonyok
DSCF0155
JAMII nchini imeaswa kuwajali watoto waishio katika mazingira magumu na wale walioko kwenye vituo vya kulelea watoto yatima kwa kuwapatia misaada mbalimbali ili waweze kuishi kama watoto wengine waishivyo majumbani
 
Rai hiyo ilitolewa jana na Meneja wa  FBME Benki LTD mkoa wa Arusha Ramadhani Lesso wakati akikabidhi misaada mbalimbali ya vyakula kwaajili ya sikukuu ya Idd El Fitiri katika vituo viwili vya kulelea  watoto yatima cha Matonyok kilichopo Olasiti na kituo cha Abu-Abdulrahamani kilichopo Jr  jijini Arusha
 
Alisema ni vyema jamii ikatambua uwepo wa watoto waishio katika mazingira magumu na wale walioko kwenye vituo, kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali kama wanavyopata watoto wa majumbani kwani ni haki yao ya msingi na kuondokana na tabia mbaya ya kuwanyanyapaa na kuwaona ni mzigo kwa jamii
 
“Tukiwajali hawa watoto hata kwa Mungu tunapata dhawabu kwani wengi wao hawajapenda kuwa katika mazingira haya,wengine wamefiwa na wazazi wao hivyo kujikuta wakiwa watoto wa mitaani”alisema Lesso
 
Aidha alitaja moja ya sababu iliyowafanya kutoa msaada huo ni pamoja na kuguswa kwa hali ya watoto waishio katika mazingira magumu hivyo kuamua kutoa faida kidogo waliyopata kama benki ili wawezekurudisha katika jamii
 
Meneja huyo alikabidhi misaada yenye dhamani ya  shilingi laki sabana na nusu katika vituo viwili ambapo kila kituo walitoa sukari,mafuta ya kupikia,mchele,sabuni za kufulia,madaftari na penseli
Mlezi katika kituo cha Matonyok kilichopo Olasiti chenye watoto(40) Bi.Emmy Sitayo  na Mlezi wa kituo cha Abu-Abdulrahamani chenye watoto(21) kilichopo Jr ,  Mama Abdulrahamani kwa nyakati tofauti walishukuru benki hiyo ya FBME kwa kuwakumbuka kipindi hichi cha sikukuu ya Idd na kuwataka makampuni na jamii kuiga mfano huo huku wakitaka  zoezi hilo liwe endelevu kwa watoto yatima na wasiojiweza.

No comments:

Post a Comment