Dr. Slaa Anaendelea Kutafuta Ufumbuzi Wa Tatizo La Kiuchumi. Makampuni yaahidi Maelfu ya Ajira!
Leo asubuhi Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mh.
Wilbrod Slaa Washington DC kuelekea jimbo la North Carolina ambako amelakiwa na
Rais wa Chuo cha Piedmond Community College yenye jumla ya campuses 16. Na
jumla ya wanafunzi 85,000
Piedmont Community College ndio moja ya Community colleges bora
zaidi Marekani, na imekuwa ikitayarisha wanafunzi mahiri kwenye eneo la engineering.
Lengo kubwa la kiongozi huyu maarufu nchini kukutana na Rais wa
Chuo, ni kujifunza siri ya mafanikio ya chuo hicho, kwa ajili ya kuwawezesha
wanafunzi wa kitanzania kufanya vizuri zaidi kwa lengo kubwa la kutayarisha
rasilimali watu. Dr. Slaa pamoja na chama cha Chadema, wanaamini kwamba, ili
kuliokoa taifa, lazima elimu ipewe nafasi ya kwanza
Kadhalika, Dr. Slaa na Rais was chuo kikuu cha Pedmont
walikubaliana kuanzisha program maalum itakayowawezesha vijana wa kitanzania na
wakimarekani kuanzisha urafiki utakaoziwezesha chuo hicho maarufu kufanya kazi
kwa ukaribu na vyuo vya kitanzania. Vyuo vya kitanzania vitanufaika zaidi hasa
kutokana na technologia ya kipekee ambayo hipo chuoni hapo
|
Dr. Slaa akipokelewa na viongozi wa Chuo Kikuu cha Central piedmont |
|
Mitambo
maalum inayotumika katika mafundisho ya viwandani. Hii ni kwa ajili ya
kuwafundisha wanafunzi wanaochukua kozi ya kuendesha mashine viwandani. |
|
Dr. Slaa akitizama kwa umakin jinsi mitambo hii ya kisasa inavyofanya kazi kati hiki chuo |
|
Dr.
Slaa Kwenye picha ya pamoja na wakuu wa mashirika makubwa
yanayotengeneza mashine nzito za ujenzi na shuguli nyingine za viwanda.
Wote wako tayari kufanya kazi Tanzania na kutengeneza maelufu ya ajira
kwa watanzania kama CHADEMA watamn'goa adui UFISADI unaoendelezwa na CCM |
|
Dr.
Slaa na Mkewe wakionyeshwa mtambo mdogo wa aina yake, ambayo inaweza
kusafisha maji machafu kwa ajili ya binadamu. Huu mtambo ni wa aina yake
na gharama nafuu sana na inaweza kutengeneza(safisha) lita 500 kwa siku
huku ikitumia mionzi ya jua yaani solar. CHADEMA itanunua hii mitambo
na kuyasambaza vijijini kupunguza tatizo la maji safi huku ikitafuta
suluhisho la kudumu |
|
Dr.
slaa pamoja na viongzi wa juu wa Charlotte Chamber of commerce kwenye
picha ya pamoja baada ya kufanya maongezi ya ushirikiano wa kibiashara |
|
Dr. Slaa akiwa kwenye maongezi na Rais wa Chuo cha Piedmont |
|
Dr.
Slaa akionyeshwa jinsi mitambo ya kisasa inayotumika katika mafunzo
inavyofanya kazi. Hii karakana ndiyo inayotumika kuwatayarisha vijana
kuwa wabunifu na kuweza kijiajiri |
|
Mitambo
maalum inayotumika katika mafundisho ya viwandani. Hii ni kwa ajili ya
kuwafundisha wanafunzi wanaochukua kozi ya kuendesha mashine viwandani. |
Baada
ya miaka 52 ya ufisadi na kuuzwa kwa rasilimali za nchi, elimu duni,
umasikini wa kupindukia, huku taifa likiendelea kuwa omba omba Dr. Slaa
pamoja na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo imeamua kutafuta njia
mbadala ya kuleta ukombozi karibu na wananchi. Chadema imeanza kutafuta
mbinu za kumkomboa mtanzania kutoka kwenye ufukara. Lengo la Chadema ni
kutengeneza mamilioni ya ajira ambazo makampuni mengi yako tayari
kuyazalisha kama Chadema itatengeneza mazingira mazuri ya wao kuwekeza.
Dr.
Slaa amemaliza ziara ya siku moja carolina na kuondoka kuelekea Atlanta
georgia ambako atakutana na viongozi wa shirika la Coca-Cola, AT&T
pamoja UPS
No comments:
Post a Comment