MAKAMU MWENYEKITI BUNGE MAALUM LA KATIBA SAMIA SULUHU KUCHUANA NA AMINA ABDALAH AMOUR
Mgombea
wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu
Hassan, ambaye ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kutoka Jimbo la Makunduchi Zanzibar. Samia kwa sasa ni Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano.
Mgombea
wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Amina
Abdallah Amour. Amina ni mjumbe kutoka Visiwani Zanzibar.
Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba wanaomuunga mkono mgombea nafasi ya Makamu
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hassan wakimsindikiza mgombea
huyo kwa hoi hoi, vifijo na nderemo kurejesha fomu yake ya kuwania
nafasi hiyo kwa Katibu wa Bunge mjini Dodoma leo.
Hapa wakitaka kumbeba mgombea wao baada ya kurejesha fomu
Wajumbe wanaomuunga mkono wakimpongeza baada ya kurejesha fomu.
Katibu
wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila akipokea fomu ya ugombea nafasi ya
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suhu Hassan jana
asabuhi kabla ya uchaguzi kufanyika jioni. Samia alikuwa akiungwa mkono
na wajumbe wengi kutoka Tanzania bara na visiwani ukilinganisha na
mpinzani wake Amina Abdalah Amour nae kutoka Zanzibar.
Mgombea nafasi ya Makamu Mwernyekiti wa Bunge la Katiba, Amina Abdallah Amour akisindikizwa na wapambe wake kurejesha fomu.
Mgombea
nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Amina Abdalah
Amour akirejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa Katibu wa Bunge, Dk.
Thomas Kashilila jana asabuhi kabla ya uchaguzi kufanyika jioni. Amina
alikuwa akichuana na mgombea mwenzake Samia Suluhu Hassan.
No comments:
Post a Comment