HABARI MPYAAA......WABUNGE 25 WA CCM, CUF, CHADEMA NA NCCR-MAGEUZI WAHAMA VYAMA VYAO NA KUJIUNGA NA CHAMA KIPYA CHA ACT
Wanasiasa
kutoka vyama mbalimbali vya siasa nchini wakiwemo wabunge 17
kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema ),wanatarajiwa
kujiunga na chama kipya cha siasa nchini, ACT -Tanzania,
kilichopata usajili wa kudumu mapema mwezi huu....
Mbali
na kuwanasa wabunge hao wa CHADEMA pia ACT -Tanzania kimefanikiwa kuwavuta
wabunge wanne kutoka chama cha Mapinduzi ( CCM ),huku kikiwa na
uhakika wa kuwachomoa wabunge watatu kutoka NNCR-Mageuzi....
Aidha
ACT- Tanzania imepiga hodi ndani ya chama cha wananchi ( CUF )
,ambapo imeshakamilisha mchakato wa kumjuimuisha kwenye safu
yao ya mapambano mbunge mmoja wa viti maalumu wa chama
hicho....
Taarifa
za uhakika kutoka ACT- Tanzania zimeweka wazi kwamba kwenye
idadi ya wabunge 17 wa CHADEMA,wabunge 6 ni wa majimbo huku
wabunge 11 wakiwa ni viti maalumu.....
Kwa
upande wa CCM,wabunge watatu watakaojiunga na ACT-Tanzania ni
wa majimbo,huku mbunge mmoja akiwa ni wa viti maalumu.Ndani ya
NNCR -Mageuzi, wabunge wote wanaotarajiwa kujiunga na chama
hicho ni wa majimbo huku baadhi ya matawi ya chama hicho
mkoani Kigoma nayo yakitajwa kuwa katika mchakato wa kugeuzwa
kuwa ofisi za ACT-Tanzania....
Katika
kuhakikisha chama hicho kinaenea katika kila kona ya
nchi,tayari kimeshajiimarisha kwenye mikoa ya
Kigoma,Rukwa,Katavi,Shinyanga,Lindi,Mtwara na Tabora ambapo
viongozi wengi waliokuwa wakikitumia CHADEMA kuanzia ngazi za
matawi hadi mikoa wameanza kufanya kazi za ACT-Tanzania....
Aidha
zipo taarifa kuwa wapo baadhi ya vigogo wa CCM akiwemo
waziri mkuu wa zamani wanatarajiwa kuwa wanachama wa chama
hicho na kwamba bado kuna mikakati inafanyika ili kuhakikisha
chama hicho kinakuwa chama chenye nguvu....
Mmoja
wa viongozi wa chama cha ACT-Tanzania ambaye hakuwa tayari
jina lake liandikwe kwa madai kuwa si msemaji wa chama
hicho,alisema kwa sasa chama kimeachwa kwa vijana ili
kukisambaza kwenye kila eneo na kwamba muda mwafaka ukifika
kitaishangaza nchi.....
Tangu
kuanzishwa kwake mapema mwaka huu,ACT- Tanzania kimeonekana kuwa
chama cha upinzani cha kupambana na CHADEMA tofauti na vyama
vingine ambavyo dhamira zao ni kuing'oa CCM madarakani....
Chama
hicho kimekuwa kikiweka matawi yake kwenye maeneo
yanayotawaliwa na CHADEMA mkoani KIGOMA na kwenye baadhi ya
mikoa nchini...
Katibu
wa ACT kanda ya magharibi,Wiston Moga alinukuliwa akisema kuwa
lengo la chama hicho ni kuleta mabadiliko kwenye ulingo wa
siasa, na wao wamedhamiria kutetea maslahi ya umma kwa lengo
la kuondoa mfumo wa maslahi binafsi ambao ni chachu ya vyama
vya siasa kushindwa kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.....
Msemaji
wa CHADEMA,Tumain Makene aliwahi kunukuliwa akisema kuwa hatua
ya chama hicho kupingana na chama chao haina mantiki kwani
kinaonekana kukosa mwelekeo mapema...
"Tunajua
lengo lao ni lipi, wanachokifanya hakitawasaidia, ni vibaraka tu
hao, nia yao ni kuidhoofisha CHADEMA, jambo ambalo hawataliweza" Alisema Makene
Kwa
upande wake katibu mkuu wa ACT,Samson Mwigamba alisema
anaamini ipo orodha ndefu ya wanachama wa vyama mbalimbali vya
siasa ambao wako tayari kujiunga na chama chao ...
Mbali
na Mwigamba, chama hicho pia kinaongozwa na Kadawi Limbu (
Mwenyekiti ),Ramadhani Ramadhan (Makamu mwenyekiti ) na Leopold
Mahona ( Naibu Katibu mkuu )
No comments:
Post a Comment