ZITTO KABWE AIJIBU KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI BAADA YA KUMTUHUMU KWA UFISADI
Hii ni kauli fupi ya Zitto Kabwe kujibu tuhuma za kambi ya upinzani zilizoelekezwa kwake.....
"Nasikitika kwamba katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu naingizwa kwenye siasa za majitaka.
"Kampuni ya LekaDutigite inamilikiwa na wasanii. Gombe Advisors ni
kampuni isiyofanya faida (Company limited by guarantee) na haina maslahi
yeyote ya kibiashara.
"Wasanii wa
Kigoma wamefanya kazi na TANAPA na NSSF, kazi ambazo zinajulikana na
zipo. Leo mpigie simu mfanyakazi yeyote wa NSSF utasikia kazi ya wasanii
hao.
"Kwa namna yeyote ile hii ni ishara ya kukosa ubinaadam
maana waliyoyasema wanajua sina faida yeyote ya kifedha Leo wala kesho
kwa LekaDutigite na Gombe Advisors.
"Kipindi ambacho mama yangu
yupo mahututi, tena mjumbe wa kamati kuu ya chama chao, pole ninayopewa
ndio hiyo. Hakuna namna ya kukosa ubinaadamu zaidi ya hivi.
"Hata hivyo, ni vema CAG afanye ukaguzi haraka sana na Mimi binafsi nitawajibika iwapo itaonekana kwa namna yeyote ile nina maslahi ya kifedha katika LekaDutigite na gombe advisors.."
No comments:
Post a Comment