Hatimaye
Mtoto Nasra Mvungi aliyefariki Juni mosi mwaka huu kufuatia kuaishi
katika matesa makubwa kutoka kwa mama yake mkubwa baada ya mama yake
kufariki na kuishi katika boksi bila huduma muhimu anazostahili kupatiwa
binadamu hasa mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja amezikwa kwa
heshima zote na wakazi wa Morogoro wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Joel
Nkaya Bendera, Mbunge wa Morogoro mjini, Abdulaziz Abood na
mfanyabiashara wa mabasi na vituo vya mafuta mkoani Morogoro Al Saed
Omary. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ametaka vyombo vya sheria Mahaka, kutoa
hukumu inayowastahili waliohusika kwa mateso na kupelekea kifo cha
Nasra.
Waombolezaji wakiwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kuaga mwili wa mtoto Nasra Mvungi.
Mfanyabiashara, Al Saed Omary aliyefanikisha kuleta mwili wa marehemu Nasra kutoka Dar es Salaam.
Waombolezaji wakiingia katika mabasi ya Abood, kwenda katika maziko.
Mazishi ya mtoto Nasra yaliendelea makaburi ya Kola mkoani Morogoro.
Mbunge
Abdulaziz Abood akiweka udongo katika kaburi la marehemu Nasra na
kuahidi kumfanyia hitma baada ya siku 40 tangu kuzikwa kwake.
Mfanyabiashara Al Saed Omar nae akiweka udongo katika kaburi la marehemu.
On Tuesday, June 03, 2014
No comments
No comments:
Post a Comment