Sunday, October 5, 2014

Jwtz lalaani vikali askari wake kushindwa kutii maelekezo ya askari wa usalama bara barani.
Jeshi la  wananchi  wa  Tanzania  JWTZ  limelaani  vikali  askari wake  kikosi   cha  kiteule   cha  nyandoto   27  KJ makoko ambaye  anadaiwa   kushindwa  kutii  maelekezo  ya  askari  polisi   wa  Usalama  Barabarani  wilayani Tarime  na  kusabisha fujo  na  vurugu  kubwa  huku  polisi  wakitumia  risasi  za  moto kudhibiti  hali  hiyo.

Akitoa  tamko  hilo  jeshi  la  wananchi  wa  Tanzania  mbele  ya  waandishi  wa  habari  mjini  Musoma, mkuu   wa   Brigedi  202  kundi  la  vikosi  kanda  ya magharibi  Brigedia  jenerali    Mathiew   Mayela  sukambi  amesema  kwa  niaba  ya  mkuu  wa  majeshi   nchini, kitendo  hicho  cha  aibu  kimefanywa  na  askari  binafsi  na  siyo  Jeshi  la  wananchi na kwamba   askari  huyo  amekiuka  kiapo  chake  hivyo  hastahili  kuendelea  kuitwa  mwanajeshi  wa  Jeshi  hilo. 
 
 kuhusu  Migogoro  ya  mipaka  kati  ya  wananchi  na  vikosi  vya Jeshi,mkuu huyo  wa  Brigedi  202  kundi  la  vikosi kanda  ya magharibi  Brigedia jenerali  sukambi,amewaonya  baadhi   ya  watu   wasipeonda  kuheshimu  mipaka  ya  vikosi   vya  jeshi.
 
 Aidha  kiongozi huyo  wa  Jeshi la  wananchi  wa  tanzania  kanda  ya magharibi,ametumia nafasi  hiyo  kuwataka   wanasiasa  kuacha  mara moja  kuingiza  masuala  ya  siasa  ndani katika  utendaji   wa  mambo  ya  kijeshi. 
 
Katika  tukio  hilo  ambalo  lilitokea  oktoba  mosi  mwaka  huu majira  ya  saa  kumi  na  moja  jioni  eneo  la  kituo cha mabasi mjini tarime, raia  mmoja  na  askari  kadhaa  wa  jeshi  la polisi  wakiongozwa  na  mkuu  wa  upelekezi  wa  makosa   ya jinai  (RCO)  kanda  maalum  ya  Tarime  Rorya  pamoja  na  askari  wawili   wa  Jeshi  la  wananchi  walijeruhiwa  kwa  risasri  wakati  wa  kuzima  vurugu  hizo.Chanzo ->http://bit.ly/1rZyp25
 

No comments:

Post a Comment