Thursday, May 5, 2016

Madiwani meru wameamua kuwasimamisha kazi watumishi hawa 3

 kutoka Halmashauri ya Meru baada ya Jana kuanza kutumbua majipu Leo jioni hii  hatimaye baraza la madiwani limewasimamisha kazi wakuu Wa tatu Wa idara Kwa ufisadi ili kupisha uchunguzi.

 Na mmoja ametupiwa virago hatakiwi kuonekana Halmashauri ya Meru 1Mkuu Wa Idara ya ardhi na maliasili Anna Muamba amekataliwa atakiwi tena. 2.Afsa mazingira Nd Ugumba amesimamishwa kupisha uchunguzi .3.Injinia Wa Wilaya amesimamishwa kupisha uchunguzi na Mtunza Azina amepewa onyo Kali .

Kwa upande wa mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki jOSHUA Nasari amesema kwamba wamekuwa wakilipigia kelele jambo hilo ilio kuhakikisha kwamba wanawaondoa viongozi wote wazembe  katika halmashauri hiyo na kwamba huo ni mwanzo na kazi inaendelea


No comments:

Post a Comment