WILAYA YA HAI YAINGIA USHIRIKIANO WA MAENDELEO NA SWEDEN
Watendaji wa Manispaa ya Arvidsjaur na halmashauri ya wilaya ya Hai wakibadilishana mkataba wa ushirikiano
Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai na wale wa Manispaa ya Arvidsjaur katika kusainiana makubaliano ya ushirikiano
Meya wa manispaa ya Arvidsjaur,Jerry Johqnsson(Katikati) akifafanua jambo baada ya kumalizika itifika ya kusaini makubaliano na hamashauri ya wilaya ya Hai,anayeshuhudia ni mwenyekiti wa halmashauri Clement Kwayu
Na Richard Mwangulube,Hai
Halmashauri
ya wilaya ya Hai,imeingia mkataba wa miaka minne wa ushirikiano na
Manispaa ya Arvidsjaur nchini Sweden unaolenga katika maeneo ya
kiuchumi na kijamii ukiwemo wa teknolojia ya kisasa ya udhibiti wa
takataka kiuchumi kwa kuziwezesha kutengezwa upya bidhaa kwa ajili ya
matumizi
Mkataba
huo ulitiwa saini wakati wa ziara ya ujumbe wa viongozi wa wilaya
ya Hai uliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya Hiyo, Novatus Makunga hivi
karibuni katika makao Makuu ya Manispaa hiyo nchini Sweden.
Wajumbe
wengine Katika ziara hiyo ya siku tano ambao ndiyo waliosaini mkataba
huo ni pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Clement
Kwayu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Melkizedeck Humbe pamoja
na Afisa Mipango wa Halmashauri Ester Mbatian
Kufuatia
mkataba huo, Halmashauri ya Wilaya ya Hai itapaswa kuandaa na
kuwasilisha katika Manispaa ya Arvidsjaur miradi mbalimbali inayolenga
katika Nyanja za biashara na viwanda vidogo na vya kati
Maeneo
mengine ya shirikiano huo ni pamoja na elimu na utoaji wa taarifa,
uboreshaji na usimamizi wa mazingira endelevu pamoja na miradi
inayolenga masuala ya ajira kwa vijana.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Hai mwishoni mwa wiki,Makunga amesema
kadhalika ushirikiano ho unalenga katika kuimarisha shughuli
mbalimbali zinazohusiana na masuala ya sekta ya utalii na utawala bora
kuanzia ngazi ya chini kabisa.
“Kwa
kushirikiana na wenzetu tunaandaa mkakati wa kuimarisha mafunzo kwa
jamii katika masuala ya uchumi na shughuli za maendeleo ya Kijamii na
lengo kubwa zaidi ni kwa kundi la vijana”. Amefafanua Makunga
Ameeleza
kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden[SIDA] ushirikiano
huo pia utatoa fursa kwa Manispaa ya Arvidsjaur kushirikiana na wilaya
ya Hai katika ujenga uwezo kwa halmashauri juu ya namna ya kupata
taarifa mbalmbali za maendeleo na kiuchumi kutoka maeneo ya vijijini
nakuzifanyia kazi.
Amesema
pia ushirikiano huo umelenga katika kuhakikisha halmashauri ya
Hai inaingia katika mfumo wa kisasa wa namna ya kusimamia ukusanyaji wa
mapato na matumizi ya fedha za maendeleo, kuboresha mawasiliano na
wadau mbalimbali ikiwemo kupitia kituo cha halmashauri hiyo cha redio
Boma FM
Amesemasa
Manispaa hiyo ya Sweden itasaidia katika ujenzi,uboreshaji na
uendelezaji wa kituo cha mafunzo kwa ajili ya maendeleo ya jamii
katika wilayani Hai pamoja na kusaidia katika kuboresha huduma za afya
Masuala
mengine yatakayotekelezwa kutokana na mahusiano hayo ni pamoja na
Manispaa ya Arvidsjaur kusaidia katika teknolojia ya urudufishaji wa
taka ambapo unawezesha taka ngumu na taka maji kuweza kutumika tena.
Makunga
amesema kuwa suala la udhibiti wa takataka ni changamoto kubwa katika
mji wa Hai ambao hauna dampo huku kukabiliwa na ongezeko la kasi la watu
wanaopenda kuweka makazi ya kuishi na kuendesha shughuli zao za kazi
Arusha,Moshi,Siha na Simanjiro.
“Kwa
wenzetu taka ni rasilimali, inachambuliwa kuanzia ngazi ya familia na
kupelekwa eneo la kutupa taka, kwa kupangwa kuangalia na aina, na
hutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali vikiwemo vikombe, vijiko, sahani
na umeme pamoja na mafuta ya kulainishia vyuma kutumika upya,”amefafanua
Ametaja
mengine ambayo yatatiliwa mkazo kutokana na ushirikiano huo ni pamoja
na Manispaa hiyo kusaidia katika kukuza uchumi na kuimarisha miundo
mbinu ya kiuchumi.
Makunga
ameeleza kuwa manispaa hiyo ambayo inamiliki uwanja wa ndege wa
kimataifa imeonyesha kuvutiwa kusaidia uimarishaji wa uwanja wa
kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) uliopo wilayani Hai kwa kuongeza
shughuli za biashara za Anga pamoja na kuboresha miundo mbinu katika
Uwanja huo
Ujumbe huo
uliweza kupata taarifa juu ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na
Manispaa hiyo zikiwemo za kuchumi, kijamii pamoja na usimamizi bora wa
ukusanyaji na matumizi ya Mapato
Kwa mujibu
wa nchi ya Sweden, Mamlaka zote za Serikali za Mitaa zinajulikana kama
Manispaa zinaongozwa kwa sheria ya bunge la nchi hiyo ambapo hivi sasa
kuna Manispaa zipatazo 260 nchini Sweden
Manispaa
hizi zinawajib wa kusimamia masuala ya elimu kuanzia ngazi ya
chekechea hadi Sekondari pamoja na kujenga na kusimamia vituo vya malezi
ya wazee na wasiojiweza
Kadhalika
manispaa hizi zinawajibu wa kusimamia vituo vya zimamoto na
uokoaji,kusimamia ujenzi na uendeshaji wa viwanja vya ndege,kusaidia
walemavu pamoja na kuunganisha wajiri na waajiriwa
Pia Makunga ameeleza kuwa Manispaa hizi zinajukumu la kusimamia vituo vya elimu ya ujasirimali kwa vijana na masuala ya Utalii ambapo Sweden kila siku hupokea watalii zaidiya 500,000 wanaotembelea vivutio mbalimbali katika Manispaa hizo kutoka nchi za ulaya
No comments:
Post a Comment