MFANYABIASHARA MAARUFU WA MADINI APIGWA RISASI ARUSHA NA KUFA PAPO HAPO.
Mwili wa Erasto Msuya na mmiliki wa SG HOTEL mkoani Arusha mara baada ya kupigwa risasi zaidi ya sita na watu wasiojulikana na kufa papo hapo.
Askari wakichunguza tukio la kupigwa kwa risasi kwa mfanya biashara huyu.
Mwili
kulia mara baada ya kupigwa risasi na kulia ni gari la kifahari aina ya
langer lover eneo linalodaiwa kupigwa risasi mfanyabiashara huyu.
Picha kwa hisani ya mdau Mutoto wa Arusha.
Habari
zilizotufikia hivi punde Kutoka chumba chetu cha habari zinaeleza kuwa
mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa Madini jijini Arusha aliyejulikana kwa
jina la Erasto Msuya na pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani humo, amepigwa risasi zaidi ya sita na watu wasiojulikana na kufa papo hapo.
Habari
zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda
BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja)
ili wakafanye biashara.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-
No comments:
Post a Comment