JAMII INATAKIWA KUELIMISHWA KUHUSU UMUHIMU WA KUZINGATIA USTAWI WA WANYAMA
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI NH DKT DAVID MATHAYO DAVID AMESEMA KWAMBA JAMII INATAKIWA KUELIMISHWA KUHUSU UMUHIMU WA KUZINGATIA USTAWI WA WANYAMA KWA LENGO LA KUPUNGUZA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NA MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI.
KAULI HIYO IMETOLEWA HII LEO KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA YA SIKU YA WANYAMA DUNIANI AMBAYO KITAIFA YAMEFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA NGARASERO HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU KATIKA MKOA WA ARUSHA
AIDHA AMESEMA KUWA NI VYEMA JAMII IKAWA KARIBU NA KUWAJENGEA MAZINGIRA MAZURI WANYAMA HAO ILI KUWEZA KUWA NA AFYA NJEMA KWANI WANAHAKI YA KUISHI
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI mh.DKT DAVID MATHAYO DAVID
KWA UPANDE WA CHRISTINA BAKUNAMI AMBAYE NI AFISA MWANDAMIZI KUTOKA WIZARA YA MAENDDELEO YA MIFUGO NA UVUVI HAPA NCHINI AMESEMA KUWA WANYAMA WAMEKUWA WAKITENDEWA VITENDO VYA KIKATILI JAMBO AMBALO LINAPUNGUZA IDADI YA WANYAMA TULIONAYIO..
MAONYESHO HAYO YAMEHUDHURIWA NA WAWAKILISHI WA BARZA LA USHAURI WA WANYAMA,MKUU WA WILAYA YA ARUMERU NYIREMBE MUNASA PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE HUKU KAULI MBIU IKISEMA KWAMBA WANYAMA WANA HAKI YA KULINDWA NAKUHESHIMIWA
No comments:
Post a Comment