Damas Makangale, Mhariri MOblog
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa
mara nyingine tena ameibuka na kauli ambao alishawahi kuitoa huko nyuma
ya viongozi wa Serikali ya awamu ya nne kushidwa kuchukua uamuzi mgumu
kwa maslahi mapana ya taifa.
Lowassa alitoa kauli hiyo mjini Dodoma
katika kikao cha bunge kinachoendelea akisema nchi inakosa viongozi
jasiri wenye kusimamia utekelezaji wa mambo waliyoamua katika Nyanja
mbalimbali za maendeleo.
"wananchi, wanasiasa, wabunge, viongozi
wanalalamika hatuwezi kuwa na jamii ya kulalamika lazima mtu mmoja
ajitokeze na kufanya maamuzi magumu lazima ajivishe joho la ujasiri ili
mambo yaende,' amesema Lowassa
Amesema nchi ina tatizo kubwa la uswahili
mwingi wa kukaa na kushidwa kutekeleza mambo yaliyoamualiwa kwenye
vikao kiasi cha kufanya kila mtu kulalamika kwa wakati wake
Lowassa amesema kuwa hata matokeo makubwa
sasa au "Big results Now" haiwezi kutekelezwa kwa sababu ya uswahili na
mazingira ya hapa Tanzania na Malaysia ni tofauti hapa ni uswahili tu
ndio unaosumbua taifa letu lishindwe kusonga mbele.
"Tukishakubaliana mambo ni lazima
yafanyike. Ni lazima tuondokane kuwa nchi ya kulalamika kuanzia kiongozi
wa juu mpaka mwananchi," alisisitiza
Sisi katika Moblog tunaungana na Lowassa
katika kutekeleza mipango ya serikali kama ilivyopangwa bila woga wala
kigugumuzi lazima viongozi wote waliopewa dhamana ya kuongoza waongoze
kwa vitendo waache uswahili ili taifa liweze kusonga mbele.
Tunakubaliana naye kwa sababu, siku za
hivi karibuni tumeona wamiliki malori wakikataa kulipa tozo ya asilimia
tano kwenye mizani ya serikali wakati sheria ya ongezeko la asilimia
hizo tano lilipitishwa na bunge na waziri mwenye dhamana John Pombe
Magufuli alikuwa sahihi kwa kusimamia sheria lakini kawa kawaida
Magufuli alipigwa stop na viongozi wake kwanini? Sheria za nchi
hazifuatwi yale yale uswahili.
Lowasa ambaye ni mbunge wa Monduli (CCM)
amesema kuwa ni vema serikali ingekuwa na mipango michache yenye
kutekelezeka na tija kwa taifa.
Aliongeza kuwa kama angekuwa kiongozi wa
serikali angejikita kwenye vipaumbele vitatu ambavyo ni ajira, Reli ya
Kati na elimu kuliko kuwa na vipaumbele vingi visivyotekelezeka.
Alibainisha kuwa tatizo kubwa
linaloifanya serikali ishindwe kufanya vizuri kwenye maeneo mbalimbali
ni kujiwekea vipaumbele vingi huku rasilimali zake zikiwa chache na
wakati mwingine zile zinazopatikana hazitumiwi vizuri.
You might also like:
No comments:
Post a Comment