SERIKALI IMEPUNGUZA ALAMA ZA UFAULU KIDATO CHA NNE NA SITA, SASA HAKUNA ALAMA 0.

DAR ES SALAAM.
ZIKIWA zimebaki siku tatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kuanza mtihani wa kumaliza ngazi hiyo ya elimu, Serikali imepunguza alama za ufaulu kwa mtihani huo pamoja na ule wa Kidato cha Sita.
ZIKIWA zimebaki siku tatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kuanza mtihani wa kumaliza ngazi hiyo ya elimu, Serikali imepunguza alama za ufaulu kwa mtihani huo pamoja na ule wa Kidato cha Sita.
Pia
imetangaza kuwa, mtihani wa taifa wa kidato cha nne na sita utakuwa na
alama 60 za ufaulu, huku alama 40 zilizobaki zitatokana na zile za
maendeleo ya mwanafunzi shuleni (CA).
Katika mfumo huo mpya, wizara hiyo pia imefuta daraja la sifuri na badala yake kutakuwa na daraja la tano.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
alitangaza uamuzi huo wa Serikali jana kwa kueleza utekelezaji wa
utaratibu huo utaanza kwenye mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka
huu.
“Hatua
hii imechukuliwa kutokana na changamoto zilizojitokeza kuanzia mwaka
2011. Tangu wakati huo kumekuwa na mabadiliko mbalimbali ambayo yamekuwa
yakifanyika,” alisema Profesa Mchome.
Alisema
kuwa, alama zilizokuwa zikitumiwa awali na Baraza la Mitihani la Taifa
(Necta) katika kupanga matokeo hayo, kwa kidato cha nne ni A=80-100,
B=65-79, C=50-64, D=35-49, F= 0-34 kwa upande wa kidato cha sita
A=80-100, B=75-79, C=65-74, D=55-64, E=45-54, S=40-44 na F= 0-39.
Alisema
mfumo mpya, umehusisha alama za kidato cha nne na cha sita na kuwa
kuanzia sasa A=75-100, B+=60-74, B=50-59, C=40-49, D=30-39, E=20-29 na
F=0-19.
“Alama
A itakuwa ni ufaulu uliojipambanua, B+ itakuwa ni ufaulu bora sana, B
ufaulu mzuri sana, C ufaulu mzuri, D ufaulu hafifu, E ufaulu hafifu sana
na F ufaulu usioridhisha kabisa,” alisema Profesa Mchome.
Alisema pia kuwa, wamebadilisha mfumo wa madaraja ambao awali kulikuwa na daraja la kwanza, la pili, la tatu, la nne na sifuri.
“Lile la sifuri tumeliondoa, badala yake kutakuwa na daraja la tano, lengo ni kuweka mlolongo mzuri zaidi,” alisema.
Alisema, alama hizo zitakuwa ni mgando (fixed grade range).
Profesa
Mchome alisema kuwa, utaratibu wa sasa wa kupanga matokeo hayo kwa
madaraja, utabadilika muda wowote kuanzia sasa na kwamba utakaokuwa
ukitumika ni ule wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Point Average
‘GPA’). MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment