Wednesday, August 7, 2013

Huyu Naye pia kaona aweke picha zake za uchi mtandaooni inasikitisha

Huyu Naye pia kaona aweke picha zake za uchi mtandaooni inasikitisha

                                                       
 Haikuwa kawaida kwa mwanamke wa kiafrika hasa mtanzania kuhusika katika matukio ya ajabu ukijaribu kumsimulia hadithi kwamba mwanamke kapiga picha za uchi bibi yako ataona unamvunjia heshima kwa sababu haikuwa tabia yao ila sasa
............. TUNAOMBA RADHI KUONYESHA PICHA HIZI ila inabidi kwa sababu kazi yetu kuonya jamii

       

MFANYABIASHARA MAARUFU WA MADINI APIGWA RISASI ARUSHA NA KUFA PAPO HAPO.

MFANYABIASHARA MAARUFU WA MADINI APIGWA RISASI ARUSHA NA KUFA PAPO HAPO.

 
Mwili wa Erasto Msuya na mmiliki wa SG HOTEL mkoani Arusha mara baada ya kupigwa risasi zaidi ya sita na watu wasiojulikana na kufa papo hapo.
 
Askari wakichunguza tukio la kupigwa kwa risasi kwa mfanya biashara huyu.
Mwili kulia mara baada ya kupigwa risasi na kulia ni gari la kifahari aina ya langer lover eneo linalodaiwa kupigwa risasi mfanyabiashara huyu. 
Picha kwa hisani ya mdau Mutoto wa Arusha.

Habari zilizotufikia hivi punde Kutoka chumba chetu cha habari zinaeleza kuwa mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa Madini jijini Arusha aliyejulikana kwa jina la Erasto Msuya na pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani humo, amepigwa risasi zaidi ya sita na watu wasiojulikana na kufa papo hapo.

Habari zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara. 

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-

BAADHI LA PICHA ZA MLIPUKO WA MOTO KATIKA UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATTA.

BAADHI LA PICHA ZA MLIPUKO WA MOTO KATIKA UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATTA.


Hii ni picha ya tukio zima la mlipuko wa moto uliotokea leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.

AWUSA YAANZISHA ULIPIAJI WA ANKARA KUPITIA MITANDAO YA SIMU

AWUSA YAANZISHA ULIPIAJI WA ANKARA KUPITIA MITANDAO YA SIMU

Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Arusha [AWUSA] wameanzisha
huduma ya kulipa bili ya malipo ya Ankara kwa wateja kupitia mitandao
yote ya simu za mikononi.

Akizungumza na Nipashe mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja  Masoud
Katiba katika maonyesho ya wakulima na wafugaji TASO nane nane,alisema
kuwa mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Arusha limeamua kuweka
huduma hiyo ili kuweza kulipa bili zake kwa wakati unaotakiwa.

Aidha alisema kuwa sababu nyingine ya kuweka huduma hiyo ni ili
kumrahisishia mteja wake katika kupunguza muda mwingi wakati wakulipa
Ankara zake,na kutembea muda mrefu kuzifuata huduma hizo na kuepukana
na usumbufu unaoweza kujitokeza.

Masoud aliongeza kuwa mitandao itakayotumika katika kurahisisha huduma
za mamlaka ni pamoja na M-PESA,TIGO PESA,AIRTEL MONEY ambapo amesema
mpaka sasa asilimia 10 ya wateja wameanza kulipia bili zao kwa kutumia
mtandao wa M-PESA ambapo amesema ndani ya mitandao yote kuna namba
maalumu ambazo mteja anaweza kuzitumia

Aidha alibainisha kuwa njia  hii itamsaidia mwanananchi kuokoa muda na
fedha nyingi ambazo alikuwa akiutumia kwa ajili ya kwenda idara ya
maji badala  yake anatumia kwa kufanyia kazi nyingine.
“tumeanzisha hii ili kumraisishia mteja kulipa bili yake kwa wakati
nabila usumbufu wowote napia na sisi kama idara ya maji tunatakiwa
tuende na wakati hasa katika kipindi hichi cha digital”alisema Masoud

Alitoa wito kwa wananchi kuepuka na usumbufu wa kwenda kulipa bili zao
za maji (Ankara)katika ofisi na badala yake watumie huduma hizi mpya.

CHADEMA WATOA TAMKO KALI JUU YA KUNG'ATUKA KWA JOHN TENDWA .....!!!

CHADEMA WATOA TAMKO KALI JUU YA KUNG'ATUKA KWA JOHN TENDWA .....!!!

John Tendwa alipaswa kuwa ameondoka kwenye Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, tangu mwaka 2008, alipofikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria. Aliendelea kufanya kazi zake hata baada ya muda wa mkataba wake alioongezewa kuwa umefikia mwisho, hivyo alikuwa anakalia ofisi hiyo ya umma, kinyume cha sheria.Ametumia muda huo wa miezi kadhaa, aliokuwa anakalia ofisi ya umma kinyume cha sheria, kuropoka na kuharibu demokrasia, kwa manufaa ya mamlaka iliyomteua na CCM. Kutokana na mwenendo (maneno na matendo) wake mbovu, CHADEMA ilitangaza kutokumpatia ushirikiano wowote, yeye kama Tendwa. Ikamtangaza kuwa adui wa demokrasia nchini.
 Kwa muda wote huo, CHADEMA ilikuwa ikitoa ushirikiano kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Badala ya kuifuta CHADEMA na kufanikisha dhamira ovu ya kuharibu amani ya nchi, ameondoka yeye.
Kuondoka kwa Tendwa hakuzuii kutekelezwa kwa mapendekezo ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, iliyomkuta na hatia ya kuvunja Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Sensa, hivyo akasababisha kutokea kwa mauaji ya Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi, Nyololo, Iringa.


Hivyo CHADEMA, kupitia Kurugenzi ya Habari na Uenezi, inataka kauli ya Rais Jakaya Kikwete juu ya utekelezaji wa mapendekezo hayo kwa Tendwa watu wengine, akiwemo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda na wote waliotajwa katika ripoti hiyo ya chombo cha serikali, kuwa walivunja sheria za nchi na kusababisha mauaji ya mwandishi, raia asiyekuwa na hatia.

Tunamkaribisha 'with benefit of doubt', msajili mpya, Jaji Francis Mutungi, kwenye kazi na majukumu yake mapya. Wapenda demokrasia na maendeleo nchini, wanamtarajia atatimiza wajibu wake kwa kuzingatia haki, sheria na utawala bora, asije akapita njia ya Tendwa.

Kupitia mchakato wa Katiba Mpya unaojadiliwa sasa hivi, CHADEMA tunapendekeza Ofisi ya Msajili ipewe uhuru zaidi na uteuzi wake, usiwe suala la Rais kuamka tu na kuamua kuteua bila wahusika kuomba, kuchujwa na kuthibitishwa na mamlaka nyingine tofauti na iliyoteua.

Tunatambua kuwa msajili mpya aliwahi kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, kwa muda mfupi, kisha akateuliwa kuwa Jaji na akateuliwa pia nafasi zingine. Na sasa mwaka mmoja baada ya kutumikia nafasi hizo, ameteuliwa kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Jaji Mutungi, anapaswa kuonesha kwa maneno na vitendo kwamba hatakuwa kama Tendwa, kwa kuanza kushughulikia matendo ya kiharamia yaliyofanywa na Green Guards wa CCM kwenye chaguzi za madiwani, zilizomalizika karibuni, ambazo si tu yalikuwa kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ambayo Jeshi la Polisi wanatakiwa kuchukua hatua, bali pia yalikuwa kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa. Hivyo yako kwenye mamlaka yake.

Jaji Mutungi, amshauri Rais Jakaya Kikwete kushughulikia mapendekezo ya Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, juu ya uvunjifu wa sheria wa wazi uliofanywa na askari polisi na John Tendwa, hivyo kusababisha mauaji ya Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi, Septemba 2, 2012, huko Nyololo, Iringa.

Aidha, Jaji Mutungi anapaswa kumshauri Rais Kikwete kujibu na kufanyia kazi barua mbili alizoandikiwa na CHADEMA juu ya kuunda Tume Huru ya Kimahakama/Kijaji, kuchunguza mauaji yaliyofanyika kwenye shughuli halali za kisiasa za CHADEMA.

Itakumbukwa kuwa mara tu baada ya mauaji mfululizo mkoani Morogoro na Iringa, CHADEMA ilimwandikia barua Rais Kikwete kumtaka aunde Tume ya Kimahakama kuchunguza utata wa vifo hivyo na vingine kadhaa vilivyotokea kwenye shughuli halali za kisiasa, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, ili ukweli ujulikane, haki itendeke na wahusika wachukuliwe hatua, hadi sasa rais hajafanya hivyo.

Itakumbukwa pia kuwa baada ya mlipuko wa bomu la Arusha, kwenye mkutano wa kampeni, CHADEMA pia ilimtaka Rais Kikwete kutumia mamlaka yake kuunda Tume Huru ya Kimahakama, ili ushahidi juu ya tukio hilo uwasilishwe, hadi sasa pia rais yuko kimya. Hivyo kwa nafasi yake, msajili mpya atoe ushauri kwa rais kuchukua hatua hizo, ili vyama vitimize wajibu wa kikatiba kufanya kazi zake kwa haki, uhuru na sheria za nchi zinazosimamia shughuli za vyama vya siasa nchini.

Imetolewa leo, Jumatatu, 5 Agosti, 2013 na;

Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari, CHADEMA

BREKING NEWS TAJIRI MKUBWA WA MADINI YA TANZANITE ERASTO APIGWA RISASI HII LEO NA KUFARIKI DUNIA

BREKING NEWS TAJIRI MKUBWA WA MADINI YA TANZANITE ERASTO APIGWA RISASI HII LEO NA KUFARIKI DUNIA

mfanyabiashara wa maaru wa madini ya Tanzanite ambeye pia ni mmiliki wa hotel ya kitali ya S.G Resort ya jijini arusha Erasto Msuya amefariki dunia leo majira ya alasiri wakati alipokuwa akitokea porini kuelekea mjini.kwa mujibu wa taarifa ambazo libeneke limezipata mara baada ya tukio hilo zinasema kuwa mfanyabiashara huyo alipigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi mara baada ya majibizano ya risasi yaliyotokea maeneo ya  barabara ya kia. Kwa habari zaidi endelea kufuatilia libeneke la kaskazini tutaendelea kuwajuza nini kinaendelea

Monday, August 5, 2013

Hebu mwangalie huyu mama mtu mzima akimwaga razi hadharani kweupe


Hebu mwangalie huyu mama mtu mzima akimwaga razi hadharani kweupe

Matukio ya kustayabisha yameendelea kutikisa dunia tukiendelea kushuhudia vitu ambavyo awali havikuwepo .kicheni pati ilikuwa ikifanyika miaka ya nyuma lakini kwa siri kubwa haikuruhusiwa mwanaume au mtoto mdogo kuhudhulia sherehe hii lakini imekuwa tofauti sana kwa siku hizi akina mama wamekuwa