WAANDISHI WA HABARI MAGAZETI YA MWANANCHI, NIPASHE NA HABARILEO WATWAA TUZO ZA ULUGURU AWARD 2013-2014 MOROGORO.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizungumza wakati wa hafla ya utoaji
wa tuzo hizo, kushoto ni Mkurugenzi wa kituo cha Maendeleo na Utamaduni,
Anthony Mhando.
Na Lilian Lucas, Morogoro.
Watu
kadhaa akiwemo mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd,
Juma Mtanda ametunukiwa tuzo ya heshima ya Uluguru Award ya mwaka
2013/14, kuhusu uandishi wa habari na upigaji picha za matukio
mbalimbali yanayogusa jamii, mkoani Morogoro.
Tuzo hiyo imetolewa na Kituo cha Maendeleo ya Utamaduni cha mjini Morogoro (Kimau).
Akitangaza
tuzo zilizotunukiwa kwa taasisi mbalimbali, Mkurugenzi wa kituo hicho,
Morogoro Anthony Mhando, alisema lengo ni kuchochea uajibikaji kwa
kufuata misingi ya utawala bora katika nyanja mbalimbali.
Mhando
alizitaja nyanja hizo kuwa ni pamoja na uandishi wa habari zinazogusa
jamii, ujasiriamali, uwekezaji, utawala bora, michezo na usanii.
Mhando
aliwataja washindi wa tuzo hizo kuwa ni pamoja na mpigapicha wa gazeti
la mwananchi mkoa wa Morogoro, Juma Mtanda aliyetwaa tuzo hizo kutokana
na mchango katika kuripoti baadhi ya habari za migogoro ya wakulima na
wafugaji, mafuriko yaliyowakumba wananchi wa la kijiji cha Magole
yaliyotokea hivi karibuni.
Wengini
waliotwaa tuzo ya uandishi wa habari ni Mwandishi Mtangazaji wa kituo
cha televisheni cha ITV ambaye ni Mwenyekiti wa Morogoro Press Club,
Idda Mushi, John Nditi kutoka TSN na Walda Magongwa wa kituo cha redio
cha Planet FM.
Kwa
upande wa viongozi utawala bora ni mbunge wa jimbo la Morogoro mjini
Abdullaziz Abood, mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera huku ngazi ya
wajasiliamali, Bacho Sadik Bacho ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha
wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA) akitwaa tuzo hiyo.
Alisema Mhando.
Kwa
upande wa taasisi za kifedha CRDB yenyewe iliibuka na tuzo ya taasisi
bora ya kifedha huku kampuni ya uwekezaji kiwanda cha kusindika tumbaku
(TLTC) wakitwaa tuzo ya kampuni bora wakati kwa upande wa michezo, jina
la Shomari Kapombe likiibuka katika soka, Cosmas Cheka ambaye ni
mwanamasumbwi, Azack Sokas aliyetwaa tuzo kupitia mchezo wa kareti.
Viongozi
wa michezo ni Zumo Makame, Awadh Komba na Paschol Kianga ambaye ni
mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) kwa wasanii Miss
Tanzania 2013 Happness Watimanya na Afande Sele anayejisghuhulisha na
muziki wa kizazi kipya huku mkuu wa mkoa wa Morogoro akiwa mgeni rasmi
katika haflas hiyo iliyofanyika ukumbi wa Mambo Club.
No comments:
Post a Comment