Wakizungumza na waandishi wa habari juzi,wanachama
hao waliogoma kutaja majina yao, walisema wamefikisha kilio chao kwa
uongozi wa CCM wa kata hiyo kwa kuwa viongozi wa kijiji wameto CCM
lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.
Walisema Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji
hicho,Edward Wazi na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Mosses Peter
wamewauzia sehemu ya malisho matajiri kutoka Arusha bila kufuata
utaratibu wa kuidhinishwa na mkutano wa kijiji.
Walisema viongozi hao wameuza maeneo ya kijiji
chao ikiwamo mapalio ya kupitishia mifugo na wakihoji kwa viongozi hao
kwa nini wameuza maeneo yao wanatishiwa kwa maneno hivyo wanashindwa
mahali pa kwenda kulalamika.
“Tumefikisha suala hilo kwa kulalamikia hadi
kwenye ofisi ya CCM ya kata,kwani viongozi hawa wa kijiji wamechaguliwa
kupitia chama kilichpo madarakani,lakini hakuna hatua zozote
zilizochukuliwa dhidi yao,” walisema wakazi hao.
Walisema maeneo hayo yaliyouzwa yaliachwa tangu
mwaka 1975 kwa ajili ya maeneo ya kupitishia na kulishia mifugo,lakini
wameshangazwa na viongozi hao kuamua kuyauza kwa wafanyabiashara hao
kutoka Arusha.
Hata hivyo,Mwenyekiti wa kijiji cha
Shambarai,Edward Wazi na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho,Mosses Peter
walikanusha vikali kuuza maeneo hayo ila walidai kuwa yameuzwa na
wamiliki husika wa maeneo hayo hivyo wao hawahusiki.
Wazi alisema maeneo hayo siyo ya Serikali ila
wamiliki wenyewe wameyauza mashamba hayo ambayo ni mali yao na wao
hawana mamlaka ya kuingilia au kutoa uamuzi juu ya mashamba hayo.
Peter alisema wamiliki hao wameyauza kihalali
mashamba hayo baada ya kupata shida, hivyo wao hawana uamuzi wa kumzuia
mtu kuuza eneo lake kwani wenyewe hawamiliki chochote na wala hawahusiki
na mashamba hayo.
No comments:
Post a Comment