Mtuhumiwa anayedaiwa kumgonga na kumuua askari wa Kikosi cha Usalama
Barabarani, Koplo Elikiza Nnko, Jackson Simbo akipandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam
jana.
Mshtakiwa huyo, alifikishwa mahakamani jana.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ladislous Komanya, alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo Machi 18 mwaka huu, katika eneo la Bamaga, Barabara ya Bagamoyo.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ladislous Komanya, alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo Machi 18 mwaka huu, katika eneo la Bamaga, Barabara ya Bagamoyo.
Wakili Komanya alidai kuwa pamoja na shtaka
hilo, mshtakiwa pia anakabiliwa na shtaka la kuingilia msafara wa
kiongozi, kinyume na sheria. Wakili alidai kuwa akiwa katika sehemu hiyo
ya Bamaga, mshtakiwa aliingilia msafara wa kiongozi na kushindwa
kuheshimu maelekezo yaliyokuwa yakitolewa kwa ishara na askari huyo.
Komanya aliendelea kudai, Simbo pia anakabiliwa
na shtaka la shindwa kutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi
hadi alipo tafutwa na vyombo vya dola.
Hata Hivyo kwa upande wake, mshtakiwa alikana
tuhuma dhidi yake na Hakimu Kwey Lusemwa aliahirisha kesi hiyo hadi
Aprili 15, mwaka huu.
Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana baada ya wakili
wake Edward Chuwa, kuomba mteja wake adhaminiwe kwa kuwa ametimiza
masharti ya dhamana.
No comments:
Post a Comment