Friday, March 8, 2013

HAYATI HUGOZ KUZIKWA LEO


Rais wa Argentina pia alifika kutoa heshima zake za mwisho kwa Chavez


Mwili wa hayati Hugo Chavez utakaushwa na kuwekwa katika makavazi ya kijeshi nchini Venezueal. Mwili wa Chavez hautazikwa kwa siku nyingine saba ili kuwaopa wananchi fursa ya kuuuona kabla ya kuzikwa.
Serikali ya Venezuela imetangaza siku saba zaidi za maombolezi kabla ya kufanyika maziko ya marehemu rais wa nchi Hito Hugo Chavez baadaye leo.
Serikali hiyo imeongeza muda wa maombolezi kufuatia kufurika zaidi watu wanaotaka kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.
Makamu wa rais , Nicolas Maduro, amesema kuwa mwili wa bwana Chavez utakaushwa na baadae kuwekwa ndani ya kaburi la vioo ambapo utakuwa ukionekana.

Amesema kuwa serikali imeamua kuchelewesha uamuzi wa mazishi yake kwasababu zaidi ya raia milioni mbili wamekuwa wakipanga mstari kwa saa nyingi kwa ajili ya kupokea jeneza la chavez linalopita.
Maafisa wanasema kuwa bwana Maduro ataapiishwa kama rais wa mpito baadaye leo na uchaguzi kufanyika baadaye.
Hugo Chavez, aliyeongoza Venezuela kwa miaka 14, alifariki baada ya kuugua Saratani kwa zaidi ya miaka miwili
.
Zaidi ya viongozi 30 kutoka nchi mbali mbali wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Chavez baadaye leo akiwemo rais wa Iran,Mahmoud Ahmadinejad, rais wa Cuba Raul Castro na rais wa Belarus Alexander Lukashenko.
Rais Ahmadinejad amemsifu Chavez kama mpigania haki na kiongozi mwenye kuleta mageuzi.
Wabune wawili wa bunge la Congress la Marekani watawakilisha nchi hiyo katika mazishi haya ikikumbukwa kuwa Chavez alikuwa mkosoaji mkubwa wa Marekani.

No comments:

Post a Comment