Tume ya uchaguzi ingali inatangaza matokeo ya urais eneo bunge moja baada ya nyingine
Mahakama ya juu nchini Kenya hii
leo itatoa uamuzi ikiwa ina uwezo wa kusikiliza kesi iliyowasilishwa
kwake na makundi ya kijamii yakitaka tume huru ya uchaguzi nchini Kenya
kusitisha shughuli ya kuhesabu kura za urais inayoendelea katika ukumbi
wa Bomas.
Makundi hayo yanadai kuwa tume inakwenda kinyume
na katiba ambayo ambayo inasema kura zinapaswa kuhesabiwa kwa njia ya
elektroniki.Hapo jana Muungano wa CORD ulielezea malalamishi kuhusu shughuli yakujumlisha kura za urais na kusema hauna imani nayo kwani ina ushahidi kuwa hujuma imefanyika wakidai wizi wa kura.
Pia wanadai kuwa katika baadhi ya maeneo, kura zilizopigwa ni nyingi kuliko idadi ya wapiga kura waliosajiliwa.
Madai haya waliyatoa hapo jana ingawa mkuu wa tume ya uchaguzi aliyakanusha vikali na kusema hakuna mahala popote ambapo wameshuhudia matokeo kuhujumiwa.
Chama hicho pia kilidai kuwa baadhi ya matokeo yalikuwa juu ikilinganishwa na idfadi ya wapiga kura.
Na kwa hilo, mkuu wa tume ya uchaguzi Isaack Hassan pia alikanusha vikali akisema hawajapata matokeo kama hayo.
Tume hiyo imesisitiza kuwa shughuli ya kuyahakiki matokeo inafanywa mbele ya maajenti wa vyama vyote.
Tume ya uchaguzi ingali inaendelea na shughuli ya kujumlisha kura za urais
Washika dau wengi walieleza wasiwasi kuhusu idadi kubwa ya kura zilizoonekana kuharibika kwani zilikuwa kura zaidi ya laki tatu. Lakini kufikia sasa zimepungua na kufika themanini.
Mkuu wa tume hiyo, Issack Hassan alisema kuwa komputa ilikuwa inaongeza idadi ya kura zilizoharibika kwa mara nane.
Shughuli ya kukusanya matokeo ilianza upya kwa mikono kufuatia matatizo haya lakini Uhuru Kenyatta angali anaongoza dhidi ya Raila Odinga.
"kulikuwa na makosa kwa namna ambavyo programu ya komputa ilikuwa imeundwa, '' alisema Hassan.
''Kwa kura zote zilizoharibika kwa kila mgombea zilikuwa zinaongezeka mara nane ,'' aliongeza kusema mwenyekiti wa tume ya uc
No comments:
Post a Comment