Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha,Isaack Joseph akizungumza na waandishi
wa habari leo katika makao makuu ya chama hicho na kudai kushangazwa na kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa,Nape Nnauye ya kuwa makundi yanayokwenda nyumbani kwa Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa,kumshawishi kugombea Urais kuwa na kusema kuwa makundi hayo ynachokifanya ni utekelezaji wa kauli ya Mwenyekiti wa CCm Taifa Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa katika sherehe za CCM mjini Songea, alipowaruhusu watu wakawashawishi wanaoona wanafaa kuwania nafasi mbalimbali.(Habari Picha na http://jamiiblog.co.tz/
Katibu Mwenezi akifafanua kuhusu kauli ya Nape na kusema “Rais alisema kama mnafikiri kuna watu wanaofaa kugombea Urais,muwafate mkawaombe,sasa napata shida kidogo sielewi watu kwenda kwa Lowasa,sijui anapoteza sifa ipi ya kuwania Urais,sioni kosa la ukiukwaji wa Kanuni,siyo vizuri kubishana na kauli ya kiongozi wako,lakini kauli hiyo kidogo hata mimi kama Mwanachama wa CCM ilinitisha”alisema Isaack Joseph
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM),Mkoa wa Arusha,Robinson Meitinyiku,akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa Habari,ambapo amekitaka Chama hicho kusimamia misingi,katiba na kanuni kwa wanachama na kukaripia wote wanaofanya makosa na kumtaka Nape kuheshimu na kutambua maadili ya utu na kumtaka atambue kuwa Lowasa ana watu nyuma yake ambao wanampenda,kumheshimu na kumjali,hivyo UVCCM hawatakaa kimya kuwasemea wanyonge wanaokwenda kumshawishi Lowasa agombee..hapo akifafanua Katiba ya CCM inavyowapa wanachama fursa ya kuwaona viongozi wao.
Katibu huyo akiendelea kufafanua jambo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari.
Kulia ni Mwandishi wa habari wa Kituo cha Radio5,Arusha Mohamed na kushoto ni Grace Macha wa Tanzania Daima,wakifuatilia mkutano huo.
Kulia ni Mwandishi wa habari wa Kituo cha Radio5,Arusha Mohamed na kushoto ni Grace Macha wa Tanzania Daima,wakifuatilia mkutano huo.
Muonekano katika ofisi ya Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha,waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali hapa nchini wakifuatilia mkutano huo.
Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Arusha kimesema hakipingani na makundi yoyote yanayokwenda kumshawishi Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowasa kuchukua fomu ya kuwania urais katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu na kusema kuwa Sauti ya watu ni Sauti ya Mungu.
Aidha Umoja wa Vijana wa CCM(Uvccm) mkoani hapa kimedai kushangazwa na kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye,ya kudai kuwa kitendo cha makundi ya watu wanaokwenda nyumbani kwa Lowasa kumshawishi agombee Urasi, hakumwondolei Lowasa sifa za kuwania urais kwa kuwa hakuna kipengele kwenye Katiba au Kanuni ya CCM kinachokataza wanacahama kufata viongozi.
Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM mkoani hapa,Isaack Joseph alipokwua akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho na kusema kuwa kimeshangazwa na kauli ya Nnauye kwani kinachofanyika ni utekelezaji wa kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa katika sherehe za CCM mjini Songea alipowaruhusu watu wakawashawishi wanaoona wanafaa kuwania urais.
Alisema kwamba kwa tabia na mila za kiafrika mtu akitembelewa na mgeni hana budi kumkaribisha ,kumkirimu pamoja na kumfanyia maandalizi yote na kusema kuwa makundi mbalimbali yameona Lowasa anafaa ndio maana yamekwenda kumshawishi agombee.
“Kama kuna makundi yanayomfuata Lowasa na yaende kwani Sauti ya watu ndio sauti ya Mungu watu wameona anafaa ndio maana wamemfuata kumshawishi sasa kunamuondoleaje sifa?”alihoji Joseph
Hatahivyo,alisema kuwa Lowasa tangu apewe adhabu ndani ya chama hicho hakuwahi kuongea lolote na hata baada ya kufunguliwa adhabu hiyo baadhi ya makundi yamekuwa yakimfuata kwa kuona anafaa na kumtaka Nnauye kuacha kuropoka hovyo.
Kwa upande mwenyekiti wa Uvccm mkoani Arusha,Robinson Meitinyiku alimshangaa Nnauye kwa kauli yake kwa kuwa katiba ya chama hicho ibara ya 14 inamruhusu mwanachama yoyote kumtembelea kiongozi wake kwa kufuata taratibu.
Alisema kuwa kuna baadhi ya makundi ambayo yamekuwa yakiwashawishi baadhi ya makada wa CCM na hata wengine kutoa sadaka na vitabu kuwanadi wagombea wao lakini hawakemewi zaidi ya Lowasa,jambo linaloonyesha Nape kuegemea upande mmoja.
Alimtahadharisha Nnauye kwamba Lowasa ni kiongozi mkubwa hapa nchini na ana wafuasi wengi nyuma yake hivyo hata wao wakiona anafaa kugombea Urais na wakipata fursa ya wkenda kumtembelea na kumshawishi wataenda.
“Lowasa ana watu wengi nyuma yake tunamheshimu na sisi kama vijana wa Arusha tuna haki zote kumtetea tutamfuata hivi karibuni kumshawishi agombee hatuwezi kukaa kimya kwa kuwa tunaona anafaa”alisem
No comments:
Post a Comment