Tuesday, March 5, 2013

MBATIA AJITOA KWENYE TUME YAKUCHUNGUZA MATOKEO MABAYA YA KIDATO CHA NNE

MWENYEKITI WA NCCR MAGEUZI MH.JAMES MBATIA


Mbatia ambaye ametajwa kuwa mmoja wa wajumbe wa tume hiyo yenye wajumbe 15, alisema kamwe hatoweza  kufanya kazi yake kwa uhuru kwa sababu  ni Mbunge wa kuteuliwa, kamati hiyo imeundwa na serikali hivyo lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi.


Mwenyekiti  wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amejitoa kwenye Tume ya serikali kuchunguza chanzo cha kushuka kwa kiwango cha kustisha cha matokeo ya kidato cha nne, iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. 
 
Mbatia ambaye ametajwa kuwa mmoja wa wajumbe wa tume hiyo yenye wajumbe 15, alisema kamwe hatoweza  kufanya kazi yake kwa uhuru kwa sababu  ni Mbunge wa kuteuliwa, kamati hiyo imeundwa na serikali hivyo lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi.
Hatua hiyo imekuja siku tatu baada ya chama hicho kumwandikia barua Rais Jakaya Kikwete, kikimuomba aunde tume ya kudumu ya elimu nchini.
Tume hiyo iliundwa kutokana na matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne,  watahiniwa 240,903 kati ya 480,036  waliofanya mtihani walipata alama sifuri, huku 23,520 sawa na asilimia 5.16 wakifaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wakipata daraja la nne.

Januari 31, mwaka huu katika kikao cha bunge, Mbatia aliwasilisha hoja binafsi kuhusu udhaifu katika sekta ya elimu akielezea kwa kina, sera ya elimu iliyopitwa na wakati, kukosekana kwa mitalaa, kuwapo kwa mihtasari mibovu ya masomo na vitabu kuwa na viwango duni.
Hata hivyo, wabunge wa CCM wakishirikiana na Serikali walimaliza hoja hiyo   bila kutolewa majibu ya msingi.
Mbatia alisema jana kuwa hawezi kufanya kazi yake kwa ufanisi ndani ya tume hiyo, kwa sababu ndiye aliwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu udhaifu sekta ya elimu,  hoja ambayo ilizimwa bila kutolewa majibu ya msingi.
“Kamati ya Waziri mkuu haina jipya la kufanya kwa sababu ipo Kamati iliyoundwa mwaka 2011 kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne,  imeeleza kila kitu na ripoti ipo ofisi ya waziri mkuu, sasa hii ya sasa inakwenda kuchunguza nini?” alihoji Mbatia.
 CHANZO MWANANCHI 

No comments:

Post a Comment