Tume huru ya
uchaguzi na mipaka nchini Kenya imekiri kuwa kulikuwa na hitilafu chungu
nzima za kimitambo, katika kutoa matangazo ya matokeo ya kura za urais
kutoka kwa vituo vya kupigia kura kote nchini.
Afisaa mkuu mtendaji wa tume hiyo,James Oswago
alielezea kuwa hitilafu hiyo ilisababishwa na kiasi kikubwa cha matokeo
yaliyokuwa yanapeperushwa moja kwa moja kutoka kwa vituo vya kupigia
kura kwa sababu ya ukosefu wa nafasi ya kutosha kwenye mitambo yake.Pia aliongeza kuwa maajenti wa wagombea wote wakuu wawili walifahamishwa kuhusu hutilafu hiyo.
Kugoma kwa muda kwa mitambo ya kupeperusha matokeo, ilisababisha hali ya wasiwasi, baada ya IEBC kusitisha kupeperusha matangazo kwa masaa kadhaa.
Maafisa wa Miungano yote ya Jubiliee na CORD, walitetea kwa sababu ya kucheleweshwa kwa matokeo na kulaumu tume ya IEBC, baada ya maafisa wake wote kuondoka katika ukumbi wa kutangazia matokeo ya urais.
Kamishna mmoja mkuu wa tume hiyo aliwataka watu kuwa watulivu akisema hakuna sababu ya watu kuwa na wasiwasi.
No comments:
Post a Comment