Friday, March 15, 2013

UN - Haki za wanawake zinatishiwa



haki za wanawake katika UN
Zaidi ya mashirika 12 ya kutetea haki za binadamu na haki za wanawake kutoka mataifa ya kiarabu yameonya kuwa azimio la UN la kukabili unyanyasaji wa wanawake linatishiwa na upinzani kutoka kwa chama cha Muslim Brotherhood kutoka Misri, uongozi wa Vatican na Urusi.
Umoja wa mataifa
Azimio hilo liko katika hatua za mwisho za mashauriano kabla ya kuidhinishwa na tume ya kutetea maslahi ya wanawake katika Umoja huo.
Muslim Brtoher hood imesema kuwa azimio hilo linatishia kuvuruga mpangilio katika jamii kwa kuwapa wanawake ruhusa ya kusafiri, kufanya kazi au hata kupanga uzazi bila idhini ya waume wao.
wanawake na haki zao
Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu kutoka mataifa ya arabuni (hasa Misri, Lebanon Palestine, Jordan na Tunisia) yametoa wito kwa mataifa yaliyo na uakilishi katika tume hiyo ya UN juu ya haki za wanawake, yakome kutumia dini, utamaduni na mila kama kisingizio cha kuruhusu ukiukaji wa haki na unyanyasaji wa wanawake.

No comments:

Post a Comment