Serikali za Sudan na Sudan
kusini zimesaini mkataba mpya wa kurejelea uchimbaji na usafirishaji wa
mafuta kutoka Sudan Kusini kupitia mabomba ya Khartoum.
Waziri wa habari wa Sudan ya kusini Barnaba Marila Benjamin, ameambia BBC kuwa nchi hizo zimeafikiana na kusaini mkataba juu ya ugawaji wa fedha za mafuta kufuatia upatanishi ulioongozwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.
Nchi hizo mbili zilitishia kuingia vitani kutokana na mvutano hasa juu ya mafuta na mipaka tangu Sudan ya Kusini ijitenge kuwa huru mwaka wa 2011.
No comments:
Post a Comment