Makadinali wafanya misa maalum |
Makadinali hao 115 watafungiwa ndani ya hekalu, bila mawasiliano na yeyote nje na wataapishwa kuweka siri ya matukio yote wakati wa uchaguzi huo. Inaaminiwa kuwa shughuli hiyo huenda ikadumu siku kadhaa.
Mwandishi wa BBC mjini Roma anasema kuwa hakuna mgombea wa wazi anayetazamiwa kuchukua mahala pa Papa mtakatifu Benedikt wa kumi na sita. Papa huyo aliwashangaza wengi alipotangaza kujiuzulu baada ya kuhudumu miaka minane. Yeye ndiye papa wa kwanza kujiuzulu katika miaka 600 iliyopita.
Maelfu ya waumini wa madhehebu ya katoliki wamekusanyika nje ya kanisa la St. Peter's Basilica, kufuatilia kwa karibu shughuli hii muhimu ya kumteua kiongozi mpya wa kanisa. Makadinali waliochaguliwa watapiga kura mara nne kwa siku hadi pale Papa mpya atakapo patikana. Kwingineko maelfu ya waumini wanatizama kwenye televisheni na kusikiliza kwenye redio matukio ya Roma kujua iwapo wamepata Papa.
Waumini washambuliwa Burundi
Watu sita wameuawa nchini Burundi kufuatia makabiliano makali kati ya polisi na na wafuasi wa mwanamke wa kanisa katoliki la Roma anayedai kuona kiwiliwili cha mama mtakatifu Maria.
Rabsha zilianza pale polisi wa Burundi walipojaribu kuwazuia wafuasi wa mwanamke huyo kwa jina Zebiya kukusanyika kwenye mlima mdogo kaskazini mwa mkoa wa Kayanza.
Idadi kubwa ya wafuasi hao pia walikamatwa. Haya ndio machafuko mabaya zaidi kutokea katika msururu wa makabiliano kati ya polisi na kitengo hicho cha Katoliki kilichojitenga kutoka kanisa kuu.
No comments:
Post a Comment