Thursday, April 11, 2013

MSAFARA WA MKUU WA WILAYA YA TANGA WAPATA AJALI WAWILI WAPOTEZA MAISHA

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu
Ajali hiyo imehusisha gari la Halmashauri ya wilaya ya Handeni ambapo watu wawili wamefariki akiwemo mwandishi wa Habari Hamis Bwanga na Afisa uhamiaji wa wilaya. 

Watu wanne wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 4.30 leo asubuhi katika kijiji cha Misima kweye barabara ya Handeni Korogwe wakiwa kwenye msafara wa kikazi kwenda vijijini kwaajili ya shughuli za upandaji wa miti kiwilaya. 


Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu amesema msafara huo ulikuwa na magari matatu ikiwemo ya kwake ambayo haijapata ajali.


Amesema gari hiyo ya halmashauri imepinduka baada ya kuacha njia na kwenda kama mita mia ambapo iliparamia jiwe na imeharibika vibaya. Kwa mujibu wa maelezo yake taarifa zaidi zitapatikana baadae kwani kwa sasa kinachofanyika ni kuwahudumia majeruhi ambao wanakimbizwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro na pia kushughulikia miili ya marehemu.




Habari hii kwachanzo kikuu vedasto mwamsungu

No comments:

Post a Comment