ZIKIWA zimebaki siku saba kabla ya kesi ya Msanii wa muziki wa Kizazi
Kipya Judith Wabura (Lady Jaydee) aliyofunguliwa na wakurugenzi wa
Clouds Media Group Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga kuanza kusikilizwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni,
Mahakama hiyo imemtaka Lady
Jaydee asizungumzie swala hilo.
Mahakama hiyo imefikia hatua hiyo kwa kuwa kesi ya msingi
inayomkabili nyota huyo wa muziki wa kizazi kipya Tanzania kuacha mpango
wake kwa sasa mpaka kesi hiyo inayotarajia kuanza kusikilizwa Mei 27
mwaka huu itakapo malizika.
Taarifa za Lady Jaydee kupigwa stop na Mahakama hiyo zimenaswa na habarimpya kutoka kwa washirika wakaribu wa Mwanadada huyo anayetamba hivi sasa na wimbo wake wa Joto Hasira.
Mbali na wadaku hao kuihabarisha Habarimpya.com, nyota huyo wa muziki
nchini Tanzania pia aliandika katika ukurasa wake wa facebook akisema
kwamba "Nadhani baada ya hii, maswali yatapungua kama sio kuisha
kabisa..."alisema Lay jaydee na kuongeza:
"Nafahamu kila mtu anasoma kwa wakati wake pengine hamkuona sababu
nilizoelezea kwanini sijatoa waraka mwingine tarehe 15 kama nilivyo
ahidi, sababu ni kuwa mahakama imesema nisizungumzie hilo suala
kwa sasa, ambapo kesi bado iko mahakamani...mpaka nitakapopewa ruhusa ya
kuzungumza au kutozungumza tena"alisema Lady Jaydee katika ukurasa wake
wa Facebook.
source--http://www.thechoicetz.com
No comments:
Post a Comment