Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB,Dk Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari,kulia ni Mkurugenzi wa Masoko,Tully Mwampamba |
Benki ya CRDB kesho itafanya semina ya siku moja kwa wanahisa wake na
kufuatiwa na Mkutano mkuu wa mwaka utakaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa
AICC jijini Arusha.
Mkurugenzi mtendaji wa CRDB,Dk Charles Kimei amesema benki
hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika soko la hisa na kuwataka wanahisa wazawa
kutouza hisa zao kwa bei chini.
Amesema tawi lilizinduliwa nchini Burundi mwishoni mwa mwaka
jana linafanya vizuri na mipango ya baadae kufungua matawi mashariki wa nchini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC)
Pia benki hiyo inajenga tawi kubwa kwenye mji wa Babati mkoa wa Manyara
ambayo ni makao makuu ya mkoa huo ambao kwa sasa unahudumiwa na Mobile
benki
http://rweyemamuinfo.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment