Wednesday, May 8, 2013

Wanaouza vipodozi wapigwa ‘stop’

Katika taarifa iliyotolewa na TFDA kwenye vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa kumekuwa na tabia ya wafanyabiashara wadogo kuuza bidhaa aina ya dawa katika vyombo vya usafiri hasa treni na mabasi ya abiria ambapo ni kinyume cha sheria.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imewapiga marufuku wafanyabiashara wa dawa na vipodozi wanaouza kwenye vyombo vya usafiri na kuwataka kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Wananchi pia wametakiwa kuacha kununua bidhaa hizo kwenye vyombo vya usafiri kutokana na ubora na usalama wake kuwa wa shaka na matumizi yake ni hatari kwa afya.
Katika taarifa iliyotolewa na TFDA kwenye vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa kumekuwa na tabia ya wafanyabiashara wadogo kuuza bidhaa aina ya dawa katika vyombo vya usafiri hasa treni na mabasi ya abiria ambapo ni kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo inaeleza kuwa dawa na vipodozi ni bidhaa zinazotengenezwa na kemikali zenye sumu zinazodhibitiwa na TFDA ambapo baadhi ya bidhaa zinatakiwa ziuzwe na kuhifadhiwa katika maeneo ambayo yanakidhi matakwa ya uhifadhi na uuzaji.
Ilieleza kuwa bidhaa hizo zikihifadhiwa katika maeneo yenye joto jingi, pachafu na pasipo na uangalizi
wowote zinakuwa duni, kushindwa kutibu na kutengeneza sumu zinazoweza kumwathiri m tumiaji.
CHANZO  MWANANCHI

No comments:

Post a Comment