MAMA MZAZI WA PROFESA JAY AGONGWA NA GARI NA KUFARIKI DUNIA
Picha kushoto ni Profesa J akiwa na mama yake
mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake...
Mama mzazi wa Msanii
Profesa Jay amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kugongwa na
gari maeneo ya mbezi juu jijini Dar alikokuwa anaishi na
mwanae.
Habari zinadai kwamba,
marehemu Bi. Rosemary Manjara Haule aligongwa na gari akiwa anavuka barabara
kuelekea dukani mida ya saa mbili na kwamba baada ya kugongwa wasamaria
wema walimkimbiza hospitali ya Tumbi kwa kutumia bajaji ambako mauti
ilimkuta huko
Profesa
Jay amethibitisha hilo na kudai kwamba ilikuwa ni vigumu sana
kuamini.Mama yake alimpigia simu na kumwambia kuwa kagongwa na gari
na kwamba yuko polisi.Ghafla simu yake ikawa haipatikani...
Profesa anasema kwamba wakati anapigiwa
simu alikuwa katika mgahawa wa nyumbani lounge,Namanga Dar ambako
alikuwa katika kikao na Lady jaydee na
mumewe.
"MAMA
ALINIAMBIA MWANANGU NIMEGONGWA NAGARI....NJONI KOPOLISINAANDIKISHA....
MWANANGU NAKUFA.... ALINIAMBIA MAMA NA MARA SIMU IKAKATIKA. KILA NILIPOJARIBU
KUPIGA IKAWA HAIPATIKANI..." ALISEMA PROFESA J KWA UCHUNGU
No comments:
Post a Comment