Monday, August 26, 2013

KATIBU MKUU WA EAC,AZUNGUMZIA MGOGORO WA RAIS KIKWETE NA RAIS KAGAME

KATIBU MKUU WA EAC,AZUNGUMZIA MGOGORO WA RAIS KIKWETE NA RAIS KAGAME

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Balozi Dk Richard Sezibera akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Arusha yalipo makao makuu ya EAC.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Daily News mkoani Arusha,Marc Nkwame akimuuliza swali Katibu Mkuu wa EAC,Dk Sezibera

Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano na Katibu Mkuu wa EAC,Dk Richard Sezibera leo


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Balozi Dk Richard Sezibera amesema mgogoro kati ya Rais wa Tanzania,Dk Jakaya Mrisho Kikwete na mwenzake wa Rwanda,Paul Kagame hauwezi kuathiri kwa kiwango cha  kuvunja  jumuiya hiyo japo sio afya kwa juhudi za mtangamano.

Amesema jitihada za kuutatua mgogoro zinafanywa na EAC pasipo kutaka kuingiliwa na vyombo vya habari na kua njia pekee ya kuumaliza ni kwanjia ya kidiplomasia.

"Tunaendelea na mashauriano ambayo hatujapenda vyombo vya habari kuingilia kwa sasa,tunaamini njia sahihi ni njia ya kidiplomasia zaidi"

Hata hivyo alikanusha taarifa zilizoenea kuwa wafanyakazi wa Tanzania na Rwanda wanaofanya kazi EAC wamekuwa hawasemeshani kutokana na mgogoro huo.

Dr Sezibera akizungumzia raia wa kigeni walioamriwa kuondoka mkoani Kagera ,alisema anaamini kila nchi ina utaratibu wake lakini hakuna sababu  ya kuwaita raia wa Afrika Mashariki wahamiaji haramu kwani wananchi wa eneo hili ni wamoja.

Alisema Kanda ya Afrika Mashariki inakabiliwa na migogoro mikubwa ukilinganisha na maeneo mengine yakiwamo makundi yaliyofanya mauji ya kimbali na mengine kama kikundi cha FNL cha Burundi na mengine jambo linalohatarisha usalama kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment