TASWAA YAANDAA TAMASHA LA NGUVU KWA VYOMBO VYA HABARI SEPTEMBA 8 MWAKA HUU ARUSHA
TAMASHA la nane la vyombo vya habari mkoa wa Arusha,
linatarajiwa kufanyika Septemba 8 katika viwanja vya General tyre Arusha na
kushirikisha waandishi kutoka jijini Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro na mkoa
wa Manyara.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa
Chama cha Waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA) Mussa Juma,
alisema zaidi ya waandishi wa habari na wadau wa habari 500
wanatarajiwa kushiriki katika Tamasha hilo.
Juma alisema kwa upande wa michezo timu ambazo
zitashiriki ni TASWA FC kutoka jijini Dar es Salaam, TASWA Arusha, Radio
Sunrise, Radio 5, Radio Triple A, Arusha One Radio na Chuo cha Uandishi wa
habari Arusha ambao ndio mabingwa watetezi.
Alisema pia kutakuwa na timu ambazo zimealikwa ambazo
ni timu ya TBL Arusha ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, timu ya Wazee
Klabu,Kitambi Noma, Timu ya Pepsi na timu ya NSSF Arusha.
Juma alisema katika tamasha hilo, ambalo huandaliwa na
TASWA na kampuni ya Ms Unique, kutakuwa na michezo ya soka, kuvuta kamba,
kukimbiza kuku, mpira wa mikono na mbio za magunia.
Alisema Septemba 7 bonanza hilo, litatanguliwa na
semina ya siku moja kwa waandishi wa habari mkoa wa Arusha kuhusiana na sheria
za michezo, masuala ya afya na jinsi ya kutumia michezo katika kutangaza
utalii.
Hata hivyo, Juma alisema bado wadhamini wanaombwa
kujitokeza kudhamini tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment