MILESTONE PARK ARUSHA NDIO MABIGWA WA SAFARI NYAMA CHOMA MKOA WA ARUSHA 2014
tuserebuke kwa ushindi jamani chezea mailstone park wewe
wafanyakazi wa mailstone wakisherekea pamoja na meneja wao alievaa nguo nyeusi mara baada ya kupokea kikombe
Mchoma nyama maarufu akiwa amebibwa na wafanyakazi wenzake wa bar ya milestone park mara baada ya kutangazwa washindi
Milestone
Park wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager
Nyama Choma 2014 yaliyofanyiaka mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa
General Tyre jijini Arusha na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi
milioni moja(1,000 000/=) na Kikombe.
Mshindi
wa pili katika fainali hizo ni QX Pub ambao walizawadiwa fedha taslimu
shilingi laki nane (800,000/=), mshindi wa tatu ni Royal Stop Over Bar
ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki sita (600,000/=), mshindi
wa nne ni New City Garden ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi
laki nne (400,000/=) na nafasi ya tano ilichukuliwa na Arusha Raha Bara
ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki mbili
(200,000/=)Akizungumza na wakazi jiji la Arusha waliohudhuria
fainalihizo, Mkuu wa Opaeshen wa jiji la hilo, ASP.Edward Balele
aliwashukuru kampuni ya bia Tanzania(TBL) kwa kuanzisha mashindano hayo
yenye mvuto wa pekee na yenye kutoa ajira na kukuza kipato kwa wachoma
nyama,lakinipia alizipongeza bar tano zilizochaguliwa kwakura za wateja
wao kuwa ni bora na kufanikiwa kushiriki fainali hizo.Alisema Balele
katunzeni na kulinda hadhi hii na kidogo mtakachopewa na Safari Lageer
kama zawadi mkakitumie vyema kuboresha majiko yenu
No comments:
Post a Comment