Monday, March 17, 2014

RIDHIWANI KIKWETE ADHAMIRIA KUWAKOMBOA WANA CHALINZE

 Kikundi cha Ngoma ya Asili ya Kizigua Kiitwacho Selo Nyota cha Kata ya Mbwewe,Bagamoyo kikitoa burudani katika moja ya Mikutano ya hadhara ya Kampeni za Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani) iliyofanyika  Machi 16,2014.

Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwa Wananchi wa Kijiji cha Kibindu,Kata ya Mbwewe,Bagamoyo  Machi 16,2014.
 Wananchi wa Kijiji cha Kwaruhombo,Kata ya Mbwewe,Bagamoyo wakiwa wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa Kijiji hicho ili kuweza kumsikiliza Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani).
 Diwani wa Kata ya Mbwewe,Omari Mhando akisisitiza jambo kwa Wananchi wa Kijiji cha Kwamuhombo wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani) uliofanyika  Machi 16,2014 kwenye Uwanja wa Kijiji hicho.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akipiga stori na vijana wa Kijiji cha Kwamduma.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akifurahi jambo kwenye moja ya mikutano yake.Kulia ni Diwani wa Kata ya Kibindu,Mkufya Ramadhan.
Wazee wakifurahia moja ya Jambo lililo wagusa.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akisalimiana na wanakijiji wa kijiji cha Kwamsanja,wakati alipofika kwa ajili ya kuzungumza nao na kuwaomba kura katika Uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment