Balozi Sief Iddi abariki tamasha la 17 la ZIFF 2014 visiwani Zanzibar
Makamu
wa Rais wa Pili wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisalimiana na
baadhi ya wageni alipowasili kwenye ufunguzi wa Tamasha la 17 la ZIFF
Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF Mh. Mahmoud Thabit Kombo.(Picha na
Zainul Mzige wa MOblog).
Mgeni
rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi
akisalimiana na Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA
"Long Walk to Freedom" Terry Pheto ambayo ilifungua tamasha hilo la 17
la ZIFF usiku wa kuamkia leo visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Wananchi Group ambao ni wadhamini wa ZIFF kupitia ZUKU, Bw. Mohammed Jeneby wakati wa tamasha hilo.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na mabalozi kwenye ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF.
Pichani juu na chini ni kikundi cha burudani cha TANURI kutoka Egypt wakitoa burudani kwenye tamasha la 17 la ZIFF.
Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando akimkaribisha mgeni Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto kwenye jukwaa.
Picha
juu na chini Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long
Walk to Freedom" Terry Pheto, akizungumzia changamoto mbalimbali na
mafanikio aliyoyapata baada ya kushiriki kwenye filamu hiyo.
Mmoja
wa wageni waalikwa akimpongeza mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa
filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto kwa kazi nzuri
aliyofanya kupitia filamu yake.
Mwenyekiti
wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha mgeni rasmi
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Sefu Iddi jukwaani kuzindua rasmi tamasha
hilo.
Mgeni
rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisoma
hotuba wakati akizindua rasmi wa Tamasha la 17 la filamu la nchi za
Majahazi (ZIFF) linaloendelea kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani
Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) akimtambulisha
mwakilishi wa Com-Net Zanzibar Bw. Mohammed (kulia) kwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi.
Mgeni
rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi
akimshukuru mwakilishi wa Com-net mmoja wa wadhamini wa tamasha hilo kwa
zawadi hiyo.
Mkurugenzi
Wananchi Group ambao ni wadhamini wa ZIFF kupitia ZUKU, Bw. Mohammed
Jeneby akizungumzia udhamini wao wa miaka 10 kwenye tamasha hilo ambapo
kwa sasa lina mwaka wa tatu.
Meza
kuu ikifuatilia filamu ya "Long Walk to Freedom" inayozungumzia maisha
ya MANDELA wakati wa ukombozi wa mtu mweusi kutoka kwa makaburu.
Mwigizaji Terry Pheto akifurahia jambo wakati wa kutazama filamu yake.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na mabalozi kwenye ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF.
Wakazi
wa Zanzibar na wageni mbalimbali kutoka nje ya Tanzania wakitazama
filamu ya "Long Walk to Freedom kwenye ukumbi wa Ngome Kongwe
linakoendelea tamasha la 17 la ZIFF.
No comments:
Post a Comment