kikundi cha akina mama kinachojulikana kwa jina la KARIAKOO WOMEN
GROUP"kilichopo jijini Arusha kimetoa zaidi ya shilingi laki tano kwa
ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto
wanaoishi katika mazingira magumu cha st Lucia kilichopo moshono jijini
hapa
Awali wakikabidhi vitu hivyo wamesema kwamba sababu iliyowapelekea kutoa
misaada hiyo ni kutokana na watoto hao kuishi katika mazingira magumu
ili kuweza kuwasaidia katika kujikwamua
Picha zikionesha akina mama hao wakikabidhi misaada hiyo kwa watoto hao{kushoto aliyeshika ndoo Elizabrth maruma akiwakabidhi
Hapa ni picha za watoto hao wakiwa pamoja na wakina mama
watoto wakifurahia chakula
wakina mama wakipata chakula
picha mbali mbali za matukio yanayojiri eneo la tukio
Ikiwa jana ni siku ya mtoto wa Africa. Uhuru wa
kupata Elimu bora bila Vikwazo. Jamii iwajibike kwenye malezi bora hasa
kutambua kuwa mtoto mwenye malezi bora anatoka kwenye familia ya kumcha
Mungu na mshikamano wa Baba na Mama.
Wazazi ili mtoto apate
elimu bora unapaswa kufwatilia maendeleo yake. Jamii tushirikiane
kwenye malezi ya watoto. Sasa tumebadilisha msemo mtoto wa mwenzio si
wako ila mume/mke wa mwenzio ndio wako ndio sababu watoto hawana malez
bora na kwenda mitaan kumbuka malez yako leo ndio maisha ya mtoto wako
kesho.
Mtoto wa mwenzio ni wako mlee kwa malezi bora ili kuepuka ukatili
kwa watoto. Hawa ni watoto yatima na wengne wana wazaz ila wako hapa
kesho watakuwa na malez gan?
Aiha kikundi hicho kina wanachama 21 ambao wana lengo la kusaidiana katika shida na raha
No comments:
Post a Comment